MOSUL, IRAK
JESHI la Irak limethibitisha kuwa wanamgambo wajiitao Dola la Kiislamu (IS) wameulipua msikiti mkuu wa Al-Nuri uliopo mjini hapa.
Msikiti huo wa kihistoria unaaminika ndimo kiongozi wa wanamgambo hao, Abu Bakr al-Baghdadi alitoa hotuba yake miaka mitatu iliyopita wakati alipokuwa akitangaza u-khalifa mpya.
Mapema jana, Jeshi la Irak lilisema askari wake walikuwa mita kadhaa kutoka msikiti huo katika harakati zao za kusonga mbele kwenye mapambano.
Lengo la jeshi hilo lilikuwa ni kujaribu kuteka ngome kuu ya wanamgambo hao.