31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Ilala yatumia Sh mil 86 kudhibiti homa za dengue

Na Christina Gauluhanga -Dar-es-salaam

MANISPAA ya Ilala imetumia Sh milioni 86 kwa awamu mbili tofauti kudhibiti homa za dengue na magonjwa mengine ya mlipuko ili kutokomeza maradhi hayo.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake juzi, Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala, Dk. Emily Lihawa alisema jitihada zimefanyika kupuliza dawa sehemu mbalimbali, hasa katika madimbwi.

Alisema awali walitumia Sh milioni 52 kununua dawa ya kungamiza viluilui wa mbu na awamu ya pili wametumia Sh milioni 34 kununua dawa nyingine za kuua mbu pevu ambayo wamepiga katika shule mbalimbali ili kutokomeza ugonjwa huo.

 Emily alisema pia tayari wamehamasisha wananchi kupima ugonjwa huo ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wameleta vifaa mbalimbali vya upimaji.

 â€śNdani ya kata 36 tumejitahidi kuhamasisha upimaji, usafishaji mazingira lengo likiwa ni kutokomeza magonjwa ya mlipuko ambapo takwimu halisi zitatolewa na wizara,” alisema Emily.

Alisema hata hivyo ugonjwa huo kwa sasa umeshuka tofauti na miaka ya 2011 /2012 ambapo ulianza na kushambuliwa wananchi kwa kasi ikiwamo watumishi wa afya.

Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, alisema hali ni shwari katika manispaa hiyo kwa kuwa kwa siku tano sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles