Ibrahimovich kurudishwa Man United

0
734

MANCHESTER, ENGLAND

KLABU ya Manchester United imeripotiwa kuwasiliana na  mshambuliaji wao wa zamani, Zlatan Ibrahimovic juu ya kumrudisha tena kwenye timu hiyo.

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38, aliondoka Old Trafford mwaka 2018 na kujiunga na klabu ya LA Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu Marekani (MLS).

Hivi karibuni mtanado wa TuttoMercatoWeb  wa nchini Italia  ulidai kuwa Mashetani Nyekundu hao wamekuwa karibu na mshambuliaji huyo wakijaribu kumrudisha kutoka Marekani.

Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer anatamani kuipata huduma ya mshmabuliaji huyo baada ya kuwauza Romelu Lukaku na Alexis Sanchez kwenda Inter Milan katika dirisha la usajili lililopita.

Licha ya Ibrahimovic, United pia ilikuwa mawindoni ku isaka saini ya mpachika mabao  wa Juventus, Mario Mandzukic  kwa lengo la kuboresha eneo la ushambuliaji.

Sasa United inaonekana kuhamishia nguvu kwa mkali huyo raia wa Sweden ambaye amekuwa na ushawishi mkubwa nje na ndani ya uwanja.

Licha ya umri wake mkubwa,Ibrahimovic aliifungia LA Galaxy mabao 31 na kuchangia upatikanaji wa mengine nane katika michezo 31 aliyoichezea timu  hiyo katika mashindano yote.

Nyota huyo wa zamani wa klabu za Ajax, Barcelona, ​​Paris Saint-Germain na AC Milan atapatikana bure Januari.

Ibrahimovic aliifungia mabao 29 katika mechi 53 baada ya kujiunga na Red Devils mwaka  2016 na kuisaidia kushinda Kombe la EFL na Ligi ya Europa.

Ripoti kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa Solskjaer yupo tayari kukabiliana na ushindani mkali  kutoka kwa Napoli na Inter Milan ambazo pia zinaitamani saini yake.

Galaxy haijakata taama ya kumuachia nyota huyo, klabu hiyo imedhamiria kumpa Pauni 6m kusaini ili kumsainisha mkataba mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here