23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Coutinho abatizwa bafuni kwake

BERLIN,Ujermani

NYOTA wa Bayern Munich, Philippe Coutinho alichagua kubatizwa kwenye bafu yake katika ubatizo wa marudio aliofanyiwa na mchungaji maarufu kutoka Brazil.
Coutinho anayeichezea timu hiyo kwa mkopo akitokea Barcelona, alifanyiwa tukio hilo pamoja na mkewe, Aine na Tiago Brunet wa kanisa la Case de Destino huko Ujerumani.
Baada ya ubatizo huo kukamilika, Coutinho aliandika kupitia akaunti yake mtandao wa kijamii : "Asante sana Mchungaji Brunet na Jeanine Brunet.
"Ilikuwa siku mbili zaidi ya maalum zilizowekwa alama katika maisha yetu, acha tuishi enzi mpya."
Wakati Coutinho akifanya ubatizo huo kwa staili ya aina yake, nyota mwenzake raia wa Brazil, Willian alitembelea Mto Yordani huko Israeli kubatizwa Juni mwakia huu.
Willian anaichezea Chelsea,  aliitikia ujumbe wa Coutinho alioutupia kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusu kubatizwa kwake kwa kuweka emoji ya mikono miwili.
Ripoti nchini Brazil hata zinaonyesha mwenye nyumba wa nyota huyo wa zamani wa Liverpool alijiunga kwenye hafla hiyo.
Mchungaji Brunet aliandika mtandao wake wa Instagram: "Siku hizi hapa Ujerumani zilikuwa za kushangaza. Karibu ndugu zetu wapya na marafiki!"
Brunet alianzisha Casa de Destino ambayo ina wafuasi zaidi ya 105,000 kwenye Instagram.
Siku ya Alhamisi iliyopita , walichapisha picha za sherehe ya Coutinho na manukuu: "Tunahubiri, tunabatiza, na tunaendelea kuwa mwanafunzi. Mungu anafanya mambo makubwa huko Ujerumani siku hizi na Tiago Brunet. Omba huduma yetu.
"Familia nzima ilipeana kwa Yesu leo
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles