28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Hussein Idd: Mfanyabiashara aliyekombolewa na mabadiliko ya kidigitali

Hussein Idd akiwasikiliza wateja.SI jambo rahisi kuamini ukiambiwa kuwa kuna wafanyabiashara wanaendesha maisha yao kwa kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao.
Unaweza kujiuliza ni kwa namna gani anaweza kupata wateja, hasa ukizingatia kuwa watu wengi nchini si wafuatiliaji wa masuala ya mitandao.
Hussein Idd ni mmoja kati ya watu wanaonufaika na biashara hiyo. Kijana huyu anaiona mitandao ya kijamii kama miongoni mwa mambo yaliyomfanya afanikiwe maishani.
Idd ni muhitimu wa fani ya Teknolojia ya Mawasiliano katika chuo cha Learn IT, anafanya biashara ya kuuza vifaa vya umeme kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Kaymu.
Mapenzi yake kwa Teknolojia ya Mawasiliano hayakuishia chuoni, bali yaliendelea hadi kuamua kufungua biashara ya kuuza vifaa vya umeme kama vile kompyuta, simu za mkononi, ‘hard drives’ na ‘flash disk” mwaka 2010. Jina la duka lake ni Jay’s Infonet Solutions.
Leo hii anauza vifaa vyake vya umeme kupitia Kaymu, kampuni ambayo ina uwezo wa kusaidia watu wengine kama yeye kufanya biashara kimataifa.
Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Idd anasema aliamua kufanya biashara kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza baada ya kuvutiwa na Kaymu.
“Nilishauriana na rafiki yangu… nilihisi kwamba kuna uhitaji wa kuwahudumia watu ambao kwa namna moja au nyingine hawana uwezo wa kufanya manunuzi kwa njia ya kawaida – kwa sababu aidha wametingwa na shughuli mbalimbali au wanafurahia tu kununua kwa njia ya mtandao na bidhaa zikaletwa mpaka nyumbani kwao bila wao kusumbuka kwenda mpaka madukani.
“Pia kupata wateja wengi waliopo ndani na nje ya nchi kwa njia ya mtandao,” anasema.
Anaelezea ni jinsi gani kuuza kwa njia ya mtandao kunaweza kuokoa muda na fedha, pia kunavyoweza kuwasaidia wauzaji na wanunuaji kufanya biashara kupitia njia salama na ya uhakika ya malipo.
“Kaymu ilinisaidia kukuza kiwango cha biashara yangu kwa kasi mno, pia imenipa fursa ya kufanya hivyo bila kutumia nguvu zaidi au uwekezaji zaidi. “Unatakiwa tu ufikirie zaidi kuhusu kitu gani unataka kuuza kupitia Kaymu – hasa vitu vinavyouzika kwa haraka zaidi ambavyo watu wanavitumia katika matumizi yao ya kila siku. Hiyo ni muhimu lakini nawashauri wafanyabiashara wenzangu kama una bidhaa nzuri, kuuza kwa njia ya mtandao kunaweza kukuletea mabadiliko makubwa,” anasema.
Anaeleza kwamba kukutana kwake kwa mara ya kwanza na Kaymu ilikuwa ni kupitia wawakilishi wa kampuni ambao walifika ofisini kwake na kumueleza jinsi mfumo wake unavyofanya kazi. “Nilishangazwa na kushawishika mno walipoanza kuzungumzia Kaymu kwa sababu sikuwahi kufikiria kwamba kampuni ya aina yoyote inaweza ikatoa huduma ya namna hii.
“Sikusita kujiunga kwa sababu nilielewa kiundani ni faida gani ingeweza kuleta kwenye biashara yangu,” anasema.
Kadri upatikanaji wa intaneti unavyokua kwa kasi na kwa bei nafuu, kuuza kwa njia ya mtandao Tanzania kumeongezeka kwa kasi ndani ya miaka miwili liliyopita.
“Najivunia kuwa mmoja kati ya wachache nchini ambao wanaongoza mabadiliko ya kidijitali Tanzania. Kwa kadri uchumi unavyoendelea kukua teknolojia nayo inakua pia, kutegemea tu biashara kwa njia ya kawaida ya rejareja kutashuka,” anasema.
Anasema matarajio yake ya kibiashara katika miaka mitano ijayo ni kwamba kwa msaada wa kutumia mfumo wa biashara kupitia Kaymu atakuwa mfanyabiashara mkubwa mno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles