23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

HUDDAH APEWA UBALOZI PUMA

NAIROBI, KENYA

MWANAMITINDO ambaye hakauki kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya, Huddah Monroe, anazidi kupiga hatua baada ya kupata dili la kuwa balozi wa kutangaza kampuni ya vifaa vya michezo vya Puma.

Wiki moja iliyopita mrembo huyo alimalizia kuuza gari yake aina ya Range Rover, hivyo aliwashangaza mashabiki wake baada ya kuiuza gari hiyo na kusema anaweza kuishi bila ya kuwa na gari, wengi walidai kuwa mrembo huyo hali yake ya uchumi imeyumba.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, amewajibu mashabiki hao kwamba bado hali yake ya uchumi ipo vizuri, lakini aliamua kuuza gari ili kubadilisha mfumo wa maisha yake.

“Hali yangu ya uchumi bado ipo vilevile na naweza kusema inazidi kukua, niliamua kuuza gari zangu kwa kuwa nilitaka kubadilisha mfumo wangu wa maisha na si kuyumba kwa uchumi, nashukuru nimepata dili la kutangaza vifaa vya michezo vya Puma, hivyo kwa sasa mimi ni balozi,” aliandika Huddah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles