23.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya Rufaa Dodoma yaanika mikakati yake

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma imetaja vipaumbele vyake kwa mwaka 2023-2024 ikiwemo kutoa huduma bora na kwa gharama ndogo.

Hayo yameelezwa leo Agosti 9,2023 na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ernest Ibenzi wakati akieleza kwa Waandishi wa Habari utekelezaji wa vipaumbele vya Hospitali hiyo kwa mwaka 2023-2024.

Dk. Ibenzi amesema vipaumbele hivyo ni kuwahudumia wananchi kwa wakati na huduma bora kwa gharama ndogo.

Pia, kutumia muda mfupi katika kumhudumia mgonjwa pamoja na uhakika wa dawa za kutosha.

“Hospitali inaendelea kukarabati na kujenga majengo kwa ajili ya kutolea huduma mbalimbali za afya,” amesema Dk. Ibenzi

Vilevile hospitali inaendelea kupiga hatua katika kutoa huduma bora kwa kuzingatia sayansi na teknolojia ya kisasa.

Pia, wanaendelea kufanya tafiti mbalimbali, kuwasomesha watumishi wa hospitali.

Dk Ibenzi amesema wanajenga jengo la gorofa 5 kwa ajili ya sehemu mbalimbali za kutolea matibabu,kuboresha mikakati ya ukusanyaji damu.

Pia,kuendelea kuboresha na kujenga miundombinu ya hospitali kwa ujumla.

Dk Ibenzi amesema Hospitali hiyo imetengewa Sh bilioni 24 kwa mwaka 2023-2024.

Amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja 2022/2023 Hospitali ilifanikiwa kufanya Kliniki tembezi katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Dodoma ambapo wagonjwa 552 walihudumiwa.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2022/2023 Idara ya Macho ilifanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa 5,319, wagonjwa waliofanyiwa upasuaji 2,234, wagonjwa 843 walipatiwa dawa.

Amesema kwa mwaka 2022/2023 Idara ya famasia imehudumia jumla ya wagonjwa 183,664, kati yao wagonjwa 83,583 walikuwa wa Bima na 100,081 wa kujitegemea.

“Wastani wa mahitaji ya damu kwa mwaka Hospitali ya Rufaa ya Dododma ni chupa/units 5,400, kipindi cha mwaka 2022/2023 chupa/Units 5,368 zilikusanywa sawa na asilimia 99% aidha, hakuna mteja aliyekosa damu,” amesema Dk. Ibenzi.

Amesema Hospitali imesimika mtambo wa gesi tiba ya hewa ya oksijeni ambapo vitanda 297 vimeunganishwa na hewa hiyo.

“Hii inasaidia kupunguza gharama za ununuaji wa gesi tiba ya hewa ya oksijeni, pia hospitali inaongeza kipato kutokana na kuuza gesi hii kwa Taasisi nyingine za afya,” amesema Dk. Ibenzi.

Amesema kati ya ukarabati na ujenzi unaofanyika kwa sasa ni pamoja na jengo la watoto ili kukabiliana na changamoto ya watoto kulala kwa kubanana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles