26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Parimatch yaidhamini Mashujaa FC

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Zikiwa zimesalia takribani siku nane kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Kampuni ya michezo ya Kubahashiri Parimatch imetangaza kuingia makubaliano ya kuidhamini Klabu ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma kwa msimu wa 2023/24.

Hafla hiyo ya kuingia udhamini imefanyika leo Agosti 10, 2023 katika Ukumbi wa Mashujaa FC ikihusisha Mkurugenzi wa Parimatch Tanzania, Erick Gerald na Uongozi wa Mashujaa.

Aidha, Erick amesema lengo mahususi la mkataba huo ni kukuza soko la mpira nchini pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.

“Parimatch tumekuwa wadau wakubwa kwenye sekta ya michezo hapa nchini na nje ya nchi na kupitia udhamini huu unalenga kusaidia timu ambayo ina vijana wanaopata ajira, wanajenga afya na kuleta ushindani kwenye michezo,” amesisitiza Erick.

Kwa upande wake kiongozi wa timu ya Mashujaa FC, Benjamin Kisinda ameishukuru Kampuni ya Parimatch Tanzania kwa kuwaamini na kuwaunga mkono katika udhamini huo ambao utawasaidia kupunguza changamoto za uendeshaji wa klabu.

“Tunawashukuru wadhamini wetu Parimatch kwa kuja kuungana nasi katika kuendeleza soka, Mashujaa ni timu ambayo imepanda daraja msimu huu, kwa hivyo tunawakaribisha sana Kigoma katika familia ya Mashujaa,” amesisitiza Kisinda.

Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya Ukaribisho ya 125% hadi kufikia Sh 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles