31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

HOSPITALI YA AMANA YATOA MASHARTI KWA WAJAWAZITO

Na Nora Damian-DAR ES SALAAM


HOSPITALI ya Rufaa Amana imeanzisha utaratibu wa wajawazito kwenda na wenzi ama ndugu zao kwa ajili ya kuchangia damu.

Mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni wastani wa chupa 350 hadi 400 kwa mwezi huku wahitaji wakubwa wakiwa ni wajawazito na watoto.

Akizungumza  wakati wa  kuchangia damu jana, Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama katika hospitali hiyo, Jabri Muhisin, alisema ingawa uchangiaji ni jambo la hiyari lakini bado watu wengi wamekuwa na hofu ya kujitokeza.

Hatua hiyo ilihusisha wafanyakazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ilala Islamic kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kiislamu ya Akhlaaqul (JAY).

“Magroup (makundi) O na Negative ndio yanayotusumbua sana kwa sababu yana watumiaji wengi, kwahiyo tumebuni mbinu ya kuwashirikisha wajawazito kuja na wenzi wao ama ndugu zao kwa ajili ya kuchangia damu,” alisema Muhsin.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilala Islamic, Buhero Issa, alisema uchangiaji damu ni mojawapo ya huduma za kijamii wanazozifanya kila mwaka kwa jamii zinazowazunguka.

“Damu ni muhimu kwa sababu inaokoa maisha ya binadamuna tumeanza kuchangia katika hospitali hii tangu mwaka juzi. Tunawahamasisha walimu na wanafunzi kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wengine,” alisema Issa.

Kwa upande wake Katibu wa Kituo cha JAY, Tawfiq Ibrahim, alisema wamekuwa wakiwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kwa kuwagharimia vipimo, dawa na kuwasafirisha wale waliomaliza matibabu yao.

Alisema pia wamekuwa wakitoa huduma ya maziko kwa watu ambao hawana ndugu na kwamba kuanzia mwaka 2012 hadi sasa wameshazika watu 198.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles