28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Hope Studio wamtambulisha Harmo Music, kusaidia chipukizi

Na Christopher Msekena, Dar es Salaam

Wadau wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini maarufu ‘Bongo Fleva’, Hope Studio wakishirikiana na Mgonja Entertainment, wamemtambulisha rasmi Msanii wao wa kwanza anayefahamika kama ‘Harmo Music.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz kuhusu ujio wa msanii huyo, Mwenyekiti wa Studio hizo zilizopo Temeke Yombo Abiola jijini Dar es Salaam, Sankawila amesema kwa kuanza wameachia wimbo wa ‘Sawa Nenda‘ ulioenda sambamba na video ya wimbo huo ikiwa ni kazi ya kwanza ya msanii Harmo Music.

“Harmo Music ni msanii wetu wa kwanza, wapo wasanii wengi ila kwa sasa tunaomba mashabiki wampe sapoti kwenye wimbo wake mpya wa ‘Sawa Nenda‘,” amesema Sankawila.

Aidha, Sankawila amewakaribisha wasanii mbalimbali kufika kwenye studio hizo kwa ajili ya kunufaika na ofa ya kurekodiwa kwa gharama nafuu pamoja na kusaidiwa kusambaza kazi husika.

“Lakini pia tunawakaribisha wasanii mbalimbali kuja kutengeneza kazi zao kwenye studio zetu za Hope Studio ambapo tunatoa ofa inayohusisha kurekodi Audio na kumsambaza kazi hiyo kwenye vituo lengo likiwa ni kusaidia vijana na kuhakikisha vipaji vyao vinakua,” amesema Sankawila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles