Home Boys yahitimisha tamasha kwa ushindi wa 2-1

0
1275

Safina Sarwatt, MoshiTAMASHA Michezo iliyokutanisha timu mbili za watani wa jadi timu ya Wazalendo Fc na Homeboys Fc  za kata ya Makuyuni Wilaya ya Moshi, mkoani  Kilimanjaro imemalizaka leo kwenye viwanja vya Mji Mdogo wa Himo huku Timu ya Homeboys ikiibuka kidedea baada ya kuinyuka Wazalendo Fc magoli 2-1.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo mwaandaji wa tamasha hilo Emmanuel Mlaki, amesema lengo la tamasha hilo ni kuzikutanisha timu hizo mbili za watani wa jadi.

“Kama mnavyofahamu leo hii mpira ni ajira, pia kupitia michezo tunajenga umoja miongoni mwetu kama  vijana na tunajenga afya za miili yetu, itakuwa ni furaha kubwa leo tukisikia kijana anayetoka hapa Makuyuni anachezea timu kubwa kama Simba au Yanga hata nje ya nchi.

“Napenda kuchukua fursa hii kusisitiza kwenu ninyi kama vijana wenzangu mbali na michezo, ni lazima tutambue fursa na nafasi yetu kama vijana katika kusaidia maendeleo ya taifa letu na Kukuza uchumi wetu binafsi,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema serikali inawathamini vijana hivyo watumie fursa hizo za michezo kama ajira.

Mshindi kwenye tamasha hilo alipata mbuzi mmoja na jezi na mshindi wa pili alijinyakulia mpira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here