23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Homa ya ini (Herpatitis B) inavyoambukiza kwa kasi – 4

hepatitis-s1-liver-hepatitis-virus

KATIKA makala zilizopita tulieleza kwa kina kuhusu ugonjwa wa homa ya ini na matibabu yake. Leo tutahitimisha kwa kuangalia dalili ambazo zinaweza kutokea na kutoweka bila matibabu.

Dalili za ugonjwa katika hatua hii zinaweza kutoweka bila matibabu

Endapo mgonjwa atakuwa na dalili za homa ya ini kwa muda mrefu, itamlazimu kupata tiba ili kuondoa tatizo japokuwa kwa watu wengine dawa hazitibu tatizo bali hulifubaza tatizo na kwa sabu hiyo wagonjwa wengine hutumia dawa katika kipindi chote cha maisha yao. Uzuri ni kwamba dawa za kutibu ugonjwa huu zipo na zinapatikana katika vidonge na sindano.

Kinga ya Hepatitis B

Jambo jema hapa ni kuwa ugonjwa huu unayo kinga. Kama tulivoangalia hapo awali ugonjwa wa homa ya ini (Hepatitis B), huambukizwa kwa njia mbali mbali. Kinga za awali zisizohitaji hata gharama ni pamoja na watu kuepuka tabia hatarishi za kimaisha ambazo ni pamoja na kujiepusha na ngono zembe, kuepuka vitendo visivyo faa vya ukahaba, ushoga, kufanya mapenzi kinyume cha maumbile, kuishi na mwenzi mmoja ama kuepuka tabia ya kubadilisha wapenzi na kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu, kuepuka tohara za mitaani, kupinga na kujiepusha na tabia za ukeketaji, kujiepusha na vitendo vya kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama nyembe, sindano, pini za kutolea funza, vifaa vya kutobolea masikio, na kuepuka matumizi ya dawa za kulevya kunakopelekea matumizi ya kujidunga sindano ambazo mara nyingi watumiaji huchagia sindano.

Shirika la afya ulimwenguni linashauri kuwa damu kabla ya kutunzwa kwenye benki ya damu, ipimwe kuangalia pamoja na magonjwa mengine ya kuambukizwa kama UKIMWI, homa ya ini ni moja ya magonjwa yanayotakiwa kuangaliwa kwa makini ili kuepuka kusambaza virusi vya HAV kutoka kwenye damu ya mtu mwenye vimelea vya mgonjwa kwenda kwa mtu asiye na vimelea vya ugonjwa wa homa ya ini hasa ikizingatiwa kuwa watu wengine huishi na vimelea vya ugonjwa bila wao kujijua kama ni waathirika.

Kinga nyingine ni chanjo ya homa ya ini. Shirika la WHO, linashauri watoto wote wapatiwe chanjo ya homa ya ini mara tu wanapozaliwa. Hapa Tanzania chanjo ya homa ya ini hutolewa kwa watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano. Mkazo hapa niutilie kwa wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya wapatiwe chanjo ya homa ya ini maana wizara ya afya hutoa chanjo hiyo bure kupitia kwa watoa huduma wake. Chanjo ya homa ini kwa Tanzania hutolewa katika chanjo muunganiko (Combined Vaccine) ambapo hupatikana kaitka chanjo tunayoita kitaalamu kama Penta vaccine (DTP-Hb+Hib) ambayo kwa pamoja humkinga motto dhidi ya magonjwa ya kifaduro, donda koo, pepopunda, homa ya Hepatitis B na homa ya mafua.

Ni jambo la faraja kuwa Serikali kupitia mpango wa chanjo huitoa chanjo hii bure kwa hiyo hakuna sababu kwa mzazi kushindwa kumkinga mwanae dhidi ya magonjwa hayo yote matano yanayopatikana katika chanjo hii. Ni vizuri pia kwa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wao wanakamilisha chanjo zote tatu ambazo hutolewa kuanzia wiki ya sita tangu motto kuzaliwa kwa chanjo ya kwanza, na baadae wiki ya kumi kwa chanjo ya pili na wiki ya kumi na nne tangu motto kuzaliwa kwa chanjo ya mwisho. Kwa mujibu wa WHO, endapo mtoto atapata chanjo zote tatu kwa muda muafaka atakuwa amekingwa kwa asilimia 95, na kwa muda miaka 20 na zaidi nap engine kumpatia kinga ya maisha.

Kwa watu watu wazima hasa wale wanaosafiri ama wale waliokatika mazingira hatarishi chanjo ya homa ya ini hutolewa peke yake, ambapo pia mtu mzima huchanjwa chanjo tatu ili kupata kinga ya muda mrefu. Watu wafuatao wanashauriwa kupata chanjo ya homa ya ini, watu wanaofanya kazi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, watu wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee, watu wanaofanya kzi katika magereza ama wafungwa, watu wanaohudumia ama kuishi na waathirika wa ugonjwa wa hepatitis B, watu wenye wapenzi ama waliowai kuwa na wapenzi wengi, watu wanaofanya kazi za maabara za binadamu, wanafanya kazi na damu mfano benki za damu, watu waliopandikizwa ini, watu wanaosafiri kuelekea nchi zenye maambukizi ama ambao wamesafiri bila kupata chanjo. Makundi haya kutokana na kuishi katika mazinnngira hatarishi yanahitaji kupata kinga ya kutosha.

Hitimisho

Tumeangalia katika mfululizo wa Makala hizi jinsi tatizo hili lilivokubwa. Wito wangu kwa wanachi ni kuchukua hatua stahiki katika kujikinga dhidi ya ugonjwa huu maana endapo watu watabadili tabia na mienendo ugonjwa huu hatari yake inaweza kupungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles