26.2 C
Dar es Salaam
Friday, December 3, 2021

Nyanya chungu hurahisisha mzunguko wa damu mwilini

nyanya-chungu

NGOGWE au nyanya chungu ni mboga ambayo inafahamika sana miongoni mwetu na baadhi yetu tumekuwa tukiitumia katika mlo lakini ni wachache wanaojua faida zake.

Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha tofauti, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu; kwanza zipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin A, B, C na K.

Madini hayo yote hufanya kazi ya kuboresha afya ya mwili kwa ujumla na kusaidia kuimarisha kinga ya mwili na hivyo kumuepusha mlaji na magonjwa ya mara kwa mara.

Baadhi ya maradhi ambayo mtu anaweza kuepukana nayo kutokana na kula nyanya chungu ni pamoja na moyo na kisukari.

Kwa upande wa Vitamin K husaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.

Mbali na sifa hizo nyanya chungu pia husaidia kuongeza stamina katika tendo la ndoa kwa muda mrefu hivyo ni tunda zuri endapo litatumiwa mara kwa mara.

Unaweza kuzitumia nyanya chungu kwa kuziunga kwenye vyakula tofauti kama vile kwa kuchanganya na mlenda, dagaa, nyama, samaki, kuku, ndizi na vingine.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,848FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles