25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Hofu ya usalama yatanda   ‘Manchester Derby’ 

mourinhoguardiola-cropped_127rrtzw3ye3m10lsno3xf3oxzLONDON, ENGLAND

KUONGEZEKA  kwa mvutano kutoka kwa mashabiki wa timu ya  Manchester united na Manchester City, kumedaiwa kuongeza hofu ya usalama  katika  mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi uwanja wa Old Trafford, England.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily mail, mchezo huo unatarajiwa kuwa chini ya ulinzi mkali wa kihistoria kila kona ya mji wa Manchester.

Uwanja huo unatarajia kuwa na polisi takribani 400 watakaoanza doria saa 12:30 usiku wakiwa katika ulinzi mkali kabla ya mchezo huo wenye upinzani mkali.

Manchester United wanatarajia kukutana na ushindani mkali tangu msimu uliopita katika mchezo dhidi ya Bournemouth ambao uliahirishwa kutokana na madai ya kuwapo kwa bomu katika uwanja  wa Old Trafford.

Wafanyakazi wa uwanja huo kwa sasa wapo katika presha kubwa ya usalama  kutokana na walinzi wa uwanja huo kufanya operesheni ya ukaguzi  kila wakati, hasa baada ya tukio dhidi ya  Bournemouth kutokea.

Mtandao wa  Daily mail unadai kwamba wataalamu  wa matukio ya kigaidi  wapo kila kona ya uwanja huo.

Moja ya lengo la kuwapo kwao ni kuzuia kutokea tena tukio la kutishia usalama tangu lilipotokea  katika mchezo dhidi ya Bournemouth.

Hata hivyo, upande wa Jeshi la Polisi wa mji huo, walithibitisha  kusimamia  kwa umakini  usalama katika mchezo huo.

“Hadi sasa hakuna  taarifa yoyote mbaya  inayotishia usalama katika mchezo huo,” kilisema chanzo kimoja cha Polisi.

Kuwapo kwa  hali ya kutoelewana  baina ya mashabiki wa timu hizo katika maeneo  mbalimbali  ambayo ni maarufu kwa starehe  katika  jiji hilo, pia  kumeongeza presha ya usalama ya mchezo huo.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho na Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, wamedaiwa kuwa katika upinzani mkubwa  zaidi ya miaka 20 iliyopita tangu wakiwa  pamoja katika  klabu ya Barcelona.

Mkuu wa  kitengo cha usalama katika jiji la Manchester, Dean Howard, alisema  mchezo huo  utakuwa  ukifuatiliwa na kila  mpenzi na shabiki wa soka duniani.

“Tuna ujuzi wa kutosha  katika matukio ya aina yoyote hivyo tupo karibu na mashabiki pamoja na wapenzi wa soka wa timu zote ili kubaini kuwapo kwa kitendo cha kutokuwa na usalama,” alisema Howard.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles