29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Serena William aweka rekodi ya  michezo 308  US Open

SERENANEW YORK, MAREKANI

BINGWA namba moja wa mchezo wa tenisi duniani  kwa upande wa wanawake, Serena Williams, jana ameweka rekodi  mpya ya kushinda  michezo  308 katika michuano mikubwa ‘Gland Slam’,  baada ya ushindi alioupata dhidi ya Yaroslava Shvedova katika michuano ya US Open inayoendelea  jijini  New York, Marekani.

Nyota huyo aliyepata ushindi dhidi ya mcheza tenisi wa Kazakhstan, Shvedova, baada ya kufikisha seti 6-2 6-3, alimpiku Roger Federe katika  orodha ya  wachezaji walioweka rekodi ya kushinda michezo  mingi kwa  muda wote katika michuano mikubwa.

Ushindi huo ulifanikisha  safari ya nyota huyo kufuzu hatua ya robo fainali ambapo kwa sasa atakutana na Mromania, Simon Halep, ambaye  alifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kumfunga Muhispania, Carla Suarez Navarro,  kwa seti 6-2 7-5.

“Ushindi wa michezo 308 ni idadi  kubwa, pia najiona nimepiga  hatua  katika kazi yangu, lakini  bado naendelea kucheza  na sijui lini nitaacha kazi hii,” alisema Serena.

“Nina furaha kuwepo hapa kwani nimeweza kuvunja rekodi ambayo sikujua kama  siku moja nitaweza kufanya hivyo,” alisema Serena.

Mbali na Serena, wachezaji wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo ni Simona Halep, Ana Konjuh, Karolina Pliskova, Caroline Wozniacki, Anastasija Sevastova, Roberta Vinci na Angelique Kerber.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles