25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Hispania yahofia kusambaratika Brexit

BRUSSELS, UBELGIJI

WAZIRI Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez amesema mzozo kuhusu eneo la Gibraltar huenda ukakwamisha mkutano maalumu wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika leo kujadili mchakato wa Uingereza kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya, mchakato unaojulikana Brexit.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani, Sanchez amesema iwapo hakutafikiwa makubaliano kuhusu eneo la Gibraltar ni wazi kuwa kujiengua kwa Uingereza hakutafanyika na kusisitiza kuwa nchi yake itatumia kura ya turufu kupinga makubaliano yaliyofikiwa kati ya Uingereza na Umoja huo.

Eneo la Gibraltar ambalo limekuwa chini ya himaya ya Uingereza tangu mwaka 1713 na Hispania inadai ni ardhi yake iko kusini mwa pwani ya nchi hiyo.

Kwa upande wake waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jana alitarajiwa kukutana na rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, Jean Claude Junker na rais wa Baraza la Umoja huo, Donald Tusk hii leo kabla ya mkutano huo wa kilele hapo kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles