22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tshisekedi awageuka wapinzani DRC

KINSHASA, DRC

HEKA HEKA za uchaguzi mkuu katika nafasi ya rais unaotarajiwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umechukua sura mpta baada ya Felix Tchisekedi kuamua kugombea kiti hicho na ushawishi wa kisiasa kama mtoto wa Marehemu Etienne Tshisekedi, mwanzilishi wa chama cha UDPS.

Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe ambao juzi walioondoa saini zao katika makubaliano ya mjini Geneva nchini Uswisi kuhusu upinzani kuwa na mgombea mmoja ambaye ni Martin Fayulu.

Hata hivyo katika hali isiyotarajiwa Felix Tshisekedi naye atakayepeperusha bendera ya upinzani ikiwa na maana kwamba kambi hiyo itakuwa na wagombea wawili.

Wagombea wote wawili wa upinzani Martin Fayulu na Felix Tshisekedi wanatarajiwa kupambana na mgombea wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila wa FCC katika Uchaguzi Mkuu  ujao mwaka huu. K

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini DRC vimesema kuwa viongozi hawa wawili wa upinzani Felix Tshisekedi wa chama cha UDPS na Vital Kamerhe wa chama cha UNC wamefikia makubaliana hayo katika mkutano unaofanyika katika hoteli Serena jijini Nairobi nchini Kenya.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki (CENCO), Donanitein Nshole amesema kuwa wana mashaka kuhusu suala la matumizi ya mashine za kupigia kura.

Kwa upande wa Alain Atundu ambaye ni msemaji wa upande wa chama tawala amesisitiza kuwa uchaguzi utakao fanyika utakuwa huru na haki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles