28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Afrika inaweza kukaribisha ‘ukoloni wa hiari’?

LONDON, UINGEREZA

MAPENDEKEZO ambayo yanatatanisha yaliyotolewa na waziri wa Ujerumani, Gunter Nooke kwamba mataifa ya kigeni yanaweza kumiliki ardhi barani Afrika ili kuzuia uhamiaji, yamepingwa vikali na Umoja wa Afrika(AU).

Umoja wa Ulaya au taasisi kama ya benki ya dunia wanapaswa kujiimarisha kwa kujenga miji barani Afrika ili kuweza kusaidia upatikanaji wa ajira na kuliendeleza bara.

Waziri wa Ujerumani katika nchi za Afrika, Gunter Nooke,aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC kwamba alipendekeza hayo kutokana na ongezeko kubwa la uhamiaji kutoka Afrika mpaka ulaya.

“Kama mataifa ya Afrika yataweza kuruhusu ardhi yao itumike kwa taasisi kubwa za kigeni ili kuwezesha bara hilo kuendelea kwa miaka 50 ijayo” alisema Nooke

Wazo hilo ambalo linatatanisha , limekosolewa na kukataliwa kwa kudaiwa kuwa ni ukoloni. Lakini wengine kama Carol Musyoka, mhadhiri wa Chuo Kikuu kimoja kikubwa nchini Kenya anaunga mkono wazo hilo.

Musyoka amelezea kuwa wazo hilo linavutia na yuko tayari kuliunga mkono kama litalenga kuhakikisha kuwa waafrika wananufaika.

Hata hivyo, mchumi kutoka Marekani ambaye ni mshindi wa tuzo ya Nobel, Paul Romer alitoa wazo hilo muongo mmoja uliopita.

Mwaka 2009, nchi zinazoendelea zinapaswa kufikiria kutoa sehemu ya eneo lake kwa mataifa ya kigeni ambayo yataweza kujenga miji ya mikataba kwa ajili ya kukuza uchumi. Aliongeza kudai kuwa miji hiyo itaendeshwa na sheria tofauti na nchi husika.

‘Hong Kong ya Marekani ya kati’

Mwaka 2008 , wakati huo rais wa Madagascar, Marc Ravalomanana alieleza namna ambavyo anavutiwa kutumia mpango huo katika visiwa vya bahari ya India.

Ravalomanana alisema miji kama hiyo miwili itajengwa eneo ambalo wananchi na wahamiaji kutoka mataifa ya jirani wanaweza kuishi.

Upande wa upinzani ulimshutumu Ravalomanana na kuandaa maandamano ambayo yaliua wazo hilo na kusababisha kuondolewa madarakani mwaka 2009.

Nchini Honduras aliyekuwa rais wa Porfirio Lobo Sosa , yeye pia aliliunga mkono wazo hilo , kwa kusema mwaka 2011 miji hiyo maalumu ya mkataba inaweza kuboresha mamia ya maisha ya watu kwa kutoa ajira zenye ushindani, huduma nzuri za afya na elimu na mfumo mzuri wa kisheria na usalama.

Gazeti moja kutoka Honduras, La Prensa liliandika kuwa ni wakati sasa wa kuweka mipango ya kuifanya nchi yao ifanane kama Hong Kong ya Marekani ya kati. Rais Sosa alishindwa kutekeleza, baada ya kukosolewa vikali na wapinzani wake.

Barani ulaya , uhamiaji ni hatari katika masuala ya kisiasa nchini Marekani na wahonduras wengi ni wahamiaji katika mpaka wa Marekani. Serikali ya sasa ya Honduras ina matumaini ya kubuni kitu kinachoitwa ukanda maalumu wa uchumi ili kukuza maendeleo.

Ingawa bado hawajaainisha mipango yao ni ipi, inasemekana kuwa mpango huo wa kukuza uchumi unaweza kuwa chini ya sheria za kigeni na kuwavutia wawekezaji wa kigeni.

“Tunaamini kuwa haya maeneo yatakayowekwa kwa ajili ya kukuza uchumi itaweza kutekelezeka na watu wataona matokeo yake chanya katika upande wa kutoa ajira na wanasiasa kutoka miji yote watahitaji mpango huo” alisema waziri wa uchumi Arnaldo Castillo.

‘Wazo halina msingi’

Uzito mkubwa upo kwa wanaopinga wazo hilo, mamia ya watu masikini wanaoishi Honduras wanaamini kwamba mpango wa kuanzisha eneo maalumu katika kuwekeza kiuchumi itaweza kuifanya jamii kuishi katika kanuni tofauti na maeneo mengine ya nchi.

Akiwa kwenye mdahalo wa TED mwaka 2011, Paul Romer uliokuwa ukijadili namna ambavyo wageni wanaweza kuiongoza miji kisasa na kutoa huduma bora na kuwafanya watu waache kuhama katika nchi zao kwa sababu za kiuchumi.

Wazo kama hilo limefanya kazi katika mji wa Hong Kong. Walihoji namna ambavyo eneo la China lilivyoweza kukuza uchumi wake wakati ilipokuwa chini ya utawala wa Uingereza mwaka 1841 mpaka 1997.

Naye waziri wa Ujerumani, Gunter anaona kuwa miji iliyojikita kibiashara inaweza kutoa elimu kwa vijana wa Afrika.

Wazo lenyewe ni kuwa miji hii huru inaweza kuleta maendeleo na mafanikio. Hata hivyo, wengine walitoa angalizo kuwa mpango huo unaweza usifanye kazi.

“Kutengeneza miji maalum ya uchumi ni wazo ambalo haliingii akilini. Miji kama hiyo utaongeza uhamiaji ndani ya nchi na hautaweza kunufaisha au kutatua tatizo ka mataifa ya Afrika. Hata kama miji hiyo haijaendelea au inakabiliana na rushwa, itakuwa vyema kama jitihada zitafanywa na taasisi za nchini mwao,” alisema Ken Opalo kutoka Chuo Kikuu cha Georgetown cha nchini Marekani.

Msemaji wa Umoja wa Afrika, Leslie Richer amelikataa wazo hilo la wageni kuongoza miji na kusema kuwa haliwezi kutekelezeka na hilo ni jibu la kivivu katika kukabiliana na uhamiaji .

Ukoloni wa hiari’

Mpango wa Umoja wa Afrika wa Agenda ya 2063 umepinga wazo hilo.

“Afrika yenyewe inaweza ikaleta miujiza katika bara lake, kwa kuimarisha ukuaji wa uchumi katika bara hilo kwa kuwa na umoja na siasa na uchumi imara”, anasema Raila Odinga.

Musyoka ni miongoni mwa waafrika wenye matumaini kuwa miji itaweza kujengwa na kukubalika kwa ukoloni wa hiari. Mawazo yake yanazika jitihada za waasisi wa bara la Afrika kutaka kuwa huru.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles