Hemed atamani kuwa mtangazaji

0
1020

NA JESSCA NANGAWE

MWIGIZAJI Hemed Suleiman ‘PHD’ ambaye pia ni msanii wa muziki nchini amefunguka na kusema ukiachia vipaji hivyo alitamani kuja kuwa mtangazaji wa TV na redio.

Akizungumza na MTANZANIA, PHD alisema pamoja na uwezo wake mzuri katika kazi zake bado anatamani siku moja aweze kutimiza ndoto yake ya utangazaji endapo atapata nafasi hiyo.

“Namshukuru Mungu sikua na kipaji cha kuigiza au kuimba tu, tangu nikiwa mdogo nilitamani sana kutangaza na niliamini ipo siku nitafanya hivyo, nadhani hata sasa nikipata nafasi hiyo nitaitumia vyema,” alisema PHD.

Alisema wapo watangazaji wengi ambao walikua wanamvutia miaka ya nyuma na kujikuta akipenda fani hiyo akiwemo Aboubakar Sadick.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here