25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Hazard hatarini kuwakosa City, Barcelona

MADRID, HISPANIA

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Real Madrid, Eden Hazard, yupo hatarini kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City wiki hii pamoja na ule wa El Clasico dhidi ya Barcelona.


Mchezaji huyo ambaye alijiunga na kikosi hicho mwishoni mwa msimu uliopita akitokea Chelsea, bado hajaonesha ubora wa kiwango chake tangu ajiunge huku akiwa anakumbwa na majeruhi ya mara kwa mara.


Staa huyo ambaye alikuwa majeruhi kwa kipindi kirefu, mwishoni mwa wiki iliopita alikuwa fiti na kupata nafasi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Levante ambapo walikubali kichapo cha bao 1-0, lakini mchezaji huyo alionekana kutolewa nje kutokana na maumivu.


Mchezaji huyo ameumia ikiwa bado siku nne timu yake kushuka dimbani kwenye mchezo dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Santiago Bernabeu ambapo ni hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Kocha wa timu hiyo Zinedine Zidane ameweka wazi kuwa, mchezaji huyo amepata tatizo ambalo linaweza kumuweka nje na kukosa baadhi ya michezo.


“Inaonekana kuwa Hazard hayupo vizuri kutokana na majeruhi aliyoyapata, lakini hatujui atakuwa nje kwa muda gani, kwa sasa tunasubiri vipimo vya madaktari,” alisema kocha huyo.


Kichapo hicho walichokipata Madrid mwishoni mwa wiki iliopita kimewapa nafasi wapinzani wao Barcelona kuongoza kwenye msimamo wa Ligi baada ya ushindi wao wa mabao 5-0 dhidi ya Eibar.


Baada ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kupigwa katikati ya wiki hii, mwishoni mwa wiki Barcelona na Real Madrid zitakutana katika mchezo wao wa marudiano hivyo kuna uwezekano wa Hazard kuukosa na huo japokuwa hadi sasa haijajulikana atakuwa nje kwa muda gani na mshindi wa mchezo huo utamfanya awe kileleni mwa msimamo wa Ligi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles