26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi ya Corona yaongezeka Korea Kusini

PYONGYANG, KOREA KUSINI

KOREA Kusini imeripoti ongezeko la maambukizi mapya ya virusi vya Corona 123 na kufanya walioambukizwa kufikia 556, wakati Italia na Iran zikichukua hatua zaidi za kukabiliana na mripuko huo.

Idadi ya vifo nchini Korea Kusini nayo imeongezeka hadi kufikia watu wanne.

Siku ya Ijumaa wili iliyomalizika jana, Italia ilikuwa nchi ya kwanza barani Ulaya kuripoti kuwa raia wake mmoja amefariki kutokana na Corona na kufuatiwa na kifo kingine juzi Jumamosi.

Zaidi ya raia 50,000 katika miji kadhaa ya Kaskazini mwa Italia wameamriwa kusalia nyumbani wakati maduka na shule vikifungwa.

Iran nayo imezifunga shule, vyuo na vituo vya utamaduni katika majimbo 14 jana, kufuatia vifo vya watu watano.

Ingawa Misri ndio taifa pekee Afrika ambalo limethibitisha kisa cha COVID-19, lakini Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilionya kuwa mifumo ya afya Afrika sio imara kuweza kukabiliana na miripuko mikubwa na kuomba ushirikiano zaidi ndani ya Umoja wa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles