Hazard awachefua mashabiki Madrid.

0
326

Kitendo cha  Eden Hazard,  kuonekana akicheka na wachezaji wa timu yake ya zamani Chelsea akiwapongeza kwa ushindi, kimewakera mashabiki wa Real Madrid.

Chelsea jana ilifanikiwa kutinga fainali ya Champions League kwa kuifunga Real Madrid mabao 2-0.

Kwa mujibu wa mtandao wa Marca, Hazard alionekana katika kamera akitaniana na kucheka na baadhi ya nyota wa Chelsea.

Kitendo hicho hakijawafurahisha mashabiki wa Madrid ambao hawajaridhishwa na hali ya kupoteza mchezo  huo wa nusu fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here