30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MAMBOSASA AWAONYA MASHABIKI WA SIMBA, YANGA

Na Brighiter Masaki

-Dar es Salaam.

Kamanda Polisi Kanda Maalimu ya Dar es Salaam, amewataka Polisi kuimarisha ulinzi Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa watani wa jadi timu ya wekundu wa msimbazi Simba na Young African Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari, mapema leo, Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika mchezo wa watani wa jadi.

“Mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga utakaochezwa uwanja wa Mkapa tarehe Mei 08, 20kujitokeza. majira ya saa 11 jioni.”

“Tumejipanga kuimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa kutosha katika maeneo yote yanayozunguka uwanja wa Mkapa na barabara zinazoingia na kutoka uwanjani hapo.”amesema Kamanda Mambosasa

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa wito kwa wazazi/walezi wanaopenda kwenda na watoto uwanjani kuwaangalia kwa karibu  au kuwaacha kabisa nyumbani ili kuepusha madhara  yoyote yanayoweza kujitokeza

Jeshi la Polisi Kanda Maalum  Dar es Salaam linatoa  wito kwa mashabiki na wapenzi wa soka  kufika uwanjani mapema ili kuepusha msongamano wakati wa kuingia uwanjani hapo kwani milango ya uwanja itafunguliwa mapema na ulinzi utakuwepo wa kutosha.

Pia tunawataka mashabiki kushangilia  kwa amani na utulivu wawapo uwanjani ikiwa ni pamoja na kuepuka mambo yafuatayo

Mihemuko na maneno ya kuhasimiana kati yao.

“Kuingia na chupa za maji majukwaani

Kuingia na silaha ya aina yoyote

Kupaki magari ndani ya uwanja pasipokuwa na kibali maalum

Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziruhusu” amesema Kamanda Mambosasa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles