24.8 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima ya kina Mbowe kufutiwa dhamana Novemba 23

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wamejisalimisha mahakamani baada ya kuamuliwa wakamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi yao.

Pamoja na kujisalimisha na kutoa maelezo kwa nini wasifutiwe dhamana, Jamhuri imewasilisha hoja za kuwabana ikiambatanisha na viapo vitatu kuonyesha washtakiwa wanaidharau mahakama, hivyo wote wafutiwe dhamana.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliiomba mahakama iwape nafasi washtakiwa wajieleze kwa nini wasifutiwe dhamana na Mbowe alikuwa wa kwanza kueleza.

Alidai anaheshimu mahakama lakini ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na nafasi zao za uongozi wanapata wakati mgumu kuweka uwiano kati ya mahakama na wajibu wao nje ya mahakama.

Alidai alisafiri Oktoba 28 kwenda Marekani na alitakiwa kurejea Oktoba 30 ili afike Dar es Salaam kesho yake lakini aliumwa na kwa mazingira ya ugonjwa wake hakuruhusiwa kusafiri kwa mwendo mrefu.

Anadai alienda kutibiwa Dubaï sababu bima yake haikumruhusu kutibiwa Marekani ingawa alipewa mapumziko lakini kwa kuiheshimu mahakama alifika jana.

“Mheshimiwa Hakimu nasumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu, ugonjwa unaohitaji umakini, unaua bila kuwapo maumivu yoyote, “alisema.

Mbowe alitoa vielelezo vya hati ya kusafiria, nyaraka za matibabu na tiketi kuonyesha mahakama kwamba aliumwa na alitibiwa Dubai.

Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori akimjibu Mbowe alidai hoja zake hazina msingi, kusafiri bila kibali cha mahakama ni kuvunja masharti ya dhamana.

Nyantori alidai mshtakiwa akiwa nje amesafiri sehemu mbalimbali na kwa ripoti aliyotoa matibabu kapata Novemba 8 mwaka huu.

Jamhuri kwa kuthibitisha kwamba Mbowe anaidharau mahakama iliwasilisha kiapo cha Kamanda wa Polisi Ilala,  Salum Hamduni, Mkaguzi wa Uhamiaji, Steven Mhina na kiapo cha Wakili, Dk. Zainabu Mangu.

Alida kiapo cha Hamduni kinaeleza kwamba Mbowe na wenzake wamekuwa na rekodi ya mara kwa mara kutokwenda kuripoti polisi kila  Ijumaa.

Nyantori alidai kiapo cha Steven kinasema ni kweli Mbowe alisafiri Oktoba 28 lakini alipohojiwa alisema anakwenda kupumzika Marekani na tiketi yake ilikuwa arudi Novemba 6 lakini hakurudi badala yake alikuwa anabadili badili tarehe za kurudi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles