30.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 7, 2021

Lema: Mawaziri hawana ubunifu sababu ya hofu

Na FREDY AZZAH-DODOMA

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema kwa sasa viongozi wa umma wakiwamo mawaziri, hawana ubunifu kwa sababu ya hofu waliyo nayo.

Lema aliyasema hayo bungeni jana wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2019/20.

“Sasa taifa lina hofu kubwa, wafanyabiashara wana hofu, Takukuru (Taasisi ya kuzui na Kupambana na Rushwa), TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) si rafiki, kwa sasa mtaji mkubwa sana unahamishwa nchini.

“Dk. Mpango (Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango), Serikali haiwezi kuendelea bila wafanyabiashara kuwa na amani, mbia namba moja wa kodi ni mfanyabiashara.

“Leo hii ukienda kila mahali wafanyabiashara wana hofu. Ukienda kwenye taasisi kuna hofu, mawaziri wana hofu, makatibu wakuu wana hofu, maendeleo yanaletwa na vitu vingi bila viongozi kujiamini hawawezi kuwa waaminifu,” alisema Lema.

Alisema katika maeneo mengine wakuu wa mikoa wanaonekana kuwa na nguvu kuliko hata mawaziri.

Lema pia alizungumzia suala  la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji na kusema polisi wamekuwa wakilifanya jambo hilo kama sinema.

“Mmeenda kutuletea sinema, yule anayeonekana kwenye picha na polisi mkisema ndiye aliyewapangishia nyumba hao watekaji ni rafiki yake Dk. Shika.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,424FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles