25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara Akram aendelea kusota rumande

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA  Akram Aziz anayekabiliwa na mashtaka 75 ya uhujumu uchumi ikiwamo ya kukutwa na nyara za serikali, silaha 70, risasi 6496 na kutakatisha fedha Dola za Marekani 9018 anaendelea kusota rumande hadi Novemba 26 mwaka huu.

Hayo yaliamuriwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizire baada ya Jamhuri kudai upelelezi haujakamilika wanaomba kuahirisha kesi.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Eliya Athanas alidai upelelezi haujakamilika anaomba tarehe nyingine ya kesi hiyo kutajwa.

Mahakama iliamuru kesi kutajwa Novemba 26 mwaka huu na mshtakiwa aendelee kuwapo rumande.

Awali, Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akimsomea mashtaka mshtakiwa, alidai anakabiliwa na mashtaka 75 alitenda makosa hayo kati ya Juni na Oktoba 30 na 31 mwaka huu maeneo ya Oysterbay.

Akisoma mashtaka Kadushi alidai mshtakiwa katika shtaka la kwanza anadaiwa Oktoba 30 mwaka huu maeneo ya Oysterbay alikutwa na meno ya tembo sita yenye thamani ya Sh 103,095,000.

Shtaka la pili mshtakiwa anadaiwa Oktoba 30 mwaka huu alikutwa na nyama ya nyati kilo 65 zenye thamani ya Dola za Marekani 1900 bila kuwa na kibali.

Kadushi alidai shtaka la tatu mpaka shtaka la 72 mshtakiwa anadaiwa kukutwa na bunduki mbalimbali aina ya rifle, bastola na shotgun bila kuwa na kibali cha mrajisi wa silaha.

Akisoma shtaka la 73 Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai Oktoba 30 mwaka huu mshtakiwa alikutwa na risasi 4092 na shtaka la 74 alikutwa na risasi 2404 Oktoba 31 mwaka huu bila kuwa na kibali.

Faraja alidai shtaka la 75, mshtakiwa anashtakiwa kwa kutakatisha fedha Dola za Marekani 9018 huku akijua ni zao la kosa tangulizi la biashara haramu ya nyara za Serikali   na kukutwa na silaha bila kibali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles