Harmonize kufungua mgahawa

0
970

Jessca Nangawe

STAA wa Bongofleva, Abdul Rajab maarafu kwa jina la Harmonize, ameweka wazi nia yake ya kutaka kufungua mgahawa wake utaojulikana kwa jina la Kondeboy Mgahawa.

Msanii huyo ambaye kwa sasa amekua gumzo kila kona, ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuthibitisha mipango hiyo.

“Hapa nilipo ni kwa neema zake Mungu, sitokula kusaza ikiwa kuna wengine kula yao ni ya shida, hivi karibuni mgahawa wangu utakujia mtaani kwako,” aliandika staa huyo kwenye Instagram.

Mbali na mgahawa, Harmonize anadaiwa yupo mbioni kumiliki kituo cha runinga cha Dira Tv ambacho kwa sasa kinamilikiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama promotions, Alex Msama.

Hii itakuwa ni sehemu moja wapo ya Harmonize kuwekeza nje ya muziki na kuungana na wasanii wengine kama vile, Diamond Platnumz, Ali Kiba na wengine wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here