August Alsina apata nafuu

0
719

NEW ORLEANS, MAREKANI

STAA wa muziki wa RnB kutoka New Orleans, Marekani, August Alsina, ameweka wazi hali ya afya yake kuwa inaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoendelea kupata.

Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya seli za damu na kumpelekea kupoteza nguvu za viungo vyake.

Alsina amekuwa akitibiwa tangu Julai mwaka huu baada ya kukutwa nyumbani kwake akiwa hawezi kutembea, lakini sasa amedai hali yake inaendelea vizuri kwa asilimia kubwa.

“Siku moja nikiwa nyumbani nilijikuta nikishindwa kutembea baada ya kuamka, jambo ambalo lilinipa wakati mgumu, lakini baada ya madaktari kuangaika kwa kila namna wakagundua nina tatizo la seli za damu, ila kwa sasa ninashukuru ninaendelea vizuri.

“Najua mashabiki wanasubiri kuona kazi zangu, hivyo ninaamini kutokana na hali inavyoendelea nitakuwa kwenye afya njema zaidi kwa siku za hivi karibuni,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here