23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Harmonize ataja wasanii levo zake

 JESSCA NANGAWE 

MKALI wa bongo fleva, Rajab Abdul maarufu kwa jina la Harmonize, amesema ni kweli msanii anatakiwa kukubali kupambanishwa lakini levo zake kwa sasa ni mastaa wakubwa kama Burna Boy wa Nigeria na wengine. 

Harmonize ambaye kwa sasa anafanya vyema kupitia lebo yake ya Konde Worldwide, alisema ushindani wa wasanii unawaweka kwenye levo nyingine ya masilahi lakini linapokuja suala hilo inabidi kuangalia wasanii wa kupambanishwa nao. 

“Nafurahi sana kupambanishwa lakini naaangalia na wasanii wenyewe, ningependa kushindanishwa na wasanii kutoka Nigeria, Ghana na kwingineko kina Burna Boy, nadhani huu ni wakati wa kubadilisha mitazamo ya watu, tushindanishwe na wasanii wa nje,” alisema Harmonize. 

Hata hivyo mkali huyo wa ngoma ya ‘Bedroom’ amefurahishwa na ushindani wa wasanii wa hapa na kudai unaleta hamasa na wasanii kujituma zaidi tofauti na walipotoka kitu ambacho ni kizuri kwa maendeleo ya muziki wao. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles