Kevin Hart ataja sababu ndoa yake kudumu

0
968

 NEW YORK, MAREKANI 

STAA wa vichekesho na filamu nchini Marekani, Kevin Hart, ametaja sababu ya ndoa yake kuto vunjika bila kujali tuhuma za kutoka na mwanamke mwingine. 

Msanii huyo alifanikiwa kufunga ndoa na Eniko Parrish mwaka 2016, lakini Desemba mwaka 2017 wawili hao waliingia kwenye mgogoro kwa madai kuwa Hart alitoka na mwanamke mwingine wakati huo mke wake akiwa na ujauzito wa mtoto wao Kenzo Kash. 

“Aliamua kuumalizi mgogoro huo kwa ushujaa, napenda kuwa sisi ni familia, haikuwa kazi rahisi kuliweka sawa jambo hilo, lakini alisimama kama mama mtarajiwa, hivyo alipambana kuzuia mambo mengine yasitoke nje. 

“Alikuwa anaipigania ndoa yake na ndio maana tupo hapa, lakini bila ya ndoa ninaamini mambo yangekuwa tofauti, naweza kusema yeye ni mwanamke bora kwangu,” alisema msanii huyo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here