28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Hapi apiga marufuku waganga wa jadi Iringa kupewa leseni

RAYMOND MINJA IRINGA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amepiga marufuku kutolewa vibalina kuwasajili waganga wa jadi kutokana na ongezeko la waganga  hao kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kila uchwao ikiwamo ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo  ambapo huenda waganga hao wakawa chanzo.

Mkoa huo,unakadiriwa kuwa  una zaidi  ya waganga wa jadi 800 waliosajiliwa huku waganga wasio na vibali wakiwa zaidi ya 500 jambo ambalo limetajwa kuwa chanzo cha matukio ya uhalifu hasa ubakaji na ulawiti kwa watoto kwa kile kinachodaiwa  waganga hao kupiga ramli chonganishi.

Akizungumza wakati wa kikao  Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC ), Hapi  alisema sasa umefika mwisho kwa waganga kuendelea kusajiliwa mkoani iringa kwani hawezi  kuwa kiongozi wa kuongoza mkoa wa waganga  wapiga ramli chonganisha na kusababisha kukatisha uhai wa watoto wasio na hatia.

“Hii kada ya kada ya waganga wa kienyeji nataka kudili nayo na sasa nasitisha utoaji wa leseni kwa waganga wote mkoani Iringa  tunataka hizi leseni 800 tuanze kwanza kushughulika nazo ili tujue wapi ni halali na wapi wasio halali kwani wapo watu ambao wanatumia huu mwanya kufanya vitu ambavyo sio sawa ikiwapo kupiga ramli chonganishi zinazokatisha uhai wa watu wetu “

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani hapa kuwachunguza waganga wote  wale wanaofanya kazi hiyo bila ya kuwa na vibali halali kutoka serekalini ili hatua ziweze kuchukulia juu yao .

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi  amewataka viongozi wa kisiasa na viongozi wa dini kushirikiana kwa pampja kukimea na kuwafichua wanaotenda maovu hayo kwani japo kuwa kuna sheria kali lakini watu wamekuwa wakiendelea kutenda maovu hayo na jamii kuwaficha .

Alisema siku za hivi karibuni  vitendo vya uwaji watoto na ubakaji vimekuwa vikiongezeka  hivyo ni jukumu la kila mtu wakiwemo wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele kuwalinda watoto.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Maji,  Juma Aweso ambaye ametumia fulsa hiyo kueleza mikakati ya wizara ya maji katika kumaliza changamoto ya maji kwa wananchi  na kuwaonya wahandisi ambao  wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles