27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Hamisa Mobetto alamba dili nono

MWANAMITINDO na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobeto ameingia mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja kuwa Balozi wa taulo za kike za Human Cherish (HQ).

Akizungumza na wandishi wa habari leo Novembaa 10, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Celine Godfrey amesema sababu ya kumchagua Mobeto ni kutokana na heshima aliyoijenga katika jamii.

“Mobeto ni msichana anaejielewa kujitambua, nidhamu yake ndio kitu pekee kilichofanya tumpe ubalozi huo wa kutangaza bidhaa yetu ya taulo za kike,” amesema Celine.

Ameongeza kuwa walifatilia mienendo ya mrembo huyo kwa kipindi kirefu wakaona ni sahihi kumpa nafasi hiyo.

Upande wake Mobeto mbali na kuishukuru kampuni hiyo pia ameahidi kuendeleza gurudumu la kusogeza kampuni hiyo karibu na jamii kwa kuwafikia hata wale walio vijijini na wasio na uwezo.

“Nina furaha kuona bidii yangu kwenye kazi zangu inaendelea kunifanya wa thamani machoni mwa watu na kuamini kunipa baadhi ya majukumu kuanzia kesho nitajua mfumo nitakao tumia kufanya kazi na kampuni hii,” amesema Mobeto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles