30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Umaskini wazidi kupungua Tanzania

Na FARAJA MASINDE

RIPOTI ya Mwenendo wa umaskini nchini iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Oktoba mwaka huu, inaonyesha kuwa umaskini umeendelea kupungua nchini.

Ripoti hiyo ambayo imeangazia hali ya umaskini kuanzia awamu ya kwanza ya uongozi inaonyesha kuwa kuemekuwa hali ya umaskini wa mahitaji ya msingi pamoja na ule wa chakula umeendelea kupungua kadri miaka inavyosonga.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa katika Serikali ya Awamu ya kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Nyerere mwaka 1964 hadi 1985, kipindi hicho, takwimu za hali ya umaskini zilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1969 na kwa mara ya pili mwaka 1977;

“Takwimu hizi hazikutumia methodolojia za kisayansi na zilifanyika kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee,” inabainisha ripoti hiyo.

Aidha, katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyoanza mwaka 1985 hadi 1995 chini ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, umaskini wa mahitaji ya msingi ulikuwa asilimia 39 huku ule wa chakula ulikuwa asilimia 22.

Kwa mujibu wa NBS, viashiria vya umaskini visivyo vya kipato, baadhi ya viashiria hivyo ni elimu, afya, hali ya makazi na vingine.

Aidha, inabainisha kuwa, kiwango cha watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 13 waliokuwa wanaosoma kilikuwa asilimia 57 pekee.

“Kwa kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa ikiongozwa na hayati, Benjamini Mkapa mwaka 1995 hadi 2005, umaskini wa mahitaji ya msingi ulikuwa asilimia 36 huku umaskini wa chakula ulikuwa asilimia 19.

“Kiwango cha watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 13 waliokuwa wanasoma kilikuwa asilimia 61, hivyo utabaini kuwa kwenye elimu kulikuwa na ongezeko la asilimia 4,” inabainisha ripoti hiyo.

Aidha, ripoti hiyo pia imechambua kuhusu awamu ya Nne ya serikali ya iliyaonza mwaka 2005 hadi 2015 chini ya Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, inayoonyesha kuwa umaskini wa mahitaji ya msing ulipungua kutoka asilimia 36 awamu ya tatu haidi asilimia 28 awamu ya Nne.

“Umaskini wa chakula ulikuwa asilimia 10; 05 na kiwango cha watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 13 waliokuwa wanaosoma kilikuwa asilimia 82 kikipanda kutoka asilimia 61 katika awamu ya Tatu,” inabainisha ripoti hiyo.

Pia, ripoti hiyo ya NBS imeangazia hali ya umaskini katika awamu ya Tano inayoongozwa na, Rais Dk. John Magufuli na kubainisha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingi ulikuwa asilimia 26.4 mwaka 2018.

“Mwaka 2020, NBS na REPOA imekadiria umaskini unapungua kwa asilimia 0.21 kwa mwaka hivyo kutoka mwaka 2017 hadi sasa umaskini umepungua hadi asilimia 25.7.

“Umaskini wa chakula ulikuwa asilimia 8.0 na kiwango cha watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 13 wanaosoma kwa mwaka 2020 ni zaidi ya asilimia 90,” inabainisha ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ya NBS inaonyesha kuwa kumekuwapo na hatua kwenye kukabiliana na umaskini ambapo inaonyesha kuwa wananchi wameendelea kupiga hatua katika kujikwamua na umaskini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles