30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri rejesheni fedha za KKK kwa wakati-Silaa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amezitaka Halmashauri zote zilizokopeshwa fedha za Kupanga, Kupima na Kumilisha (KKK) Ardhi nchi kurejesha fedha hizo kwa wakati ili waweze kukopeshwa wengine.

Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo desemba wilayani Musoma mkoa wa Mara wakati akiongea na Viongozi wa Kamati ya Usalama wa mkoa na maafisa wa sekta ya ardhi katika ziara yake ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Vijiji 975 nchini.

Silaa amezitaka Halmashauri hizo baada ya kuona halmshauri nyingi zinakopeshwa fedha hizo ambazo kazi yake ni Kupanga, Kupima na Kumilikisha viwanja kwa wananchi lakini zimekuwa hazirejeshwi kwa wakati.

Amesema, kuchelewa kurejeshwa kwa mikopo hiyo inakwamisha mzunguko wa fedha hizo ambazo wengine wanazihitaji na zinakwamisha juhudi za kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha, amesema katika kukomesha hali hiyo Wizara yake imeamua kuanzisha akaunti ya pamoja ambayo itakuwa inafanya ufuatiliaji wa fedha hizo katika matumizi na kurejeshwa kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles