31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Silaa: Msiwapangie wananchi ukubwa wa viwanja wananvyotaka

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amewataka wataalamu wa ardhi nchini kutokuwapangia wananchi ukubwa wa viwanja wanavyotaka kununua.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wilayani Musoma mkoa wa Mara wakati Desemba 11, akiongea na Viongozi wa Kamati ya Usalama wa mkoa na maafisa wa sekta ya ardhi katika ziara yake ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu Migogoro ya Vijiji 975 nchini.

Waziri Silaa amewataka wataalamu wa ardhi kushirikiana na wananchi ili kuwasaidia katika upimaji shirikishi unaofanywa na makampuni binafsi katika mitaa yao.

Amesema kila mtu awe huru kununua ukubwa wa kiwanja kutokana na uwezo wake na asipangiwe kama makampuni ya upangaji yanavyofanya ili kuepuka uwepo wa viwanja vodogovidogo katika maeneo yetu.

Aidha, Silaa amewataka wataalamu wa ardhi kutokuwa madalali wa wapima viwanja badala yake kuwapa uelewa na kuwasaidia wananchi kufahamu gharama za upimaji kwa mita za mraba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles