22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

HALIMA MDEE AMWOMBA RADHI SPIKA

Spika wa Bunge, Job Ndugai

 

Na ELIZABETH HOMBO-DODOMA

ZIKIWA zimepita siku takriban 21, tangu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuagiza Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kufika bungeni ndani ya saa 24 vinginevyo akamatwe na polisi kutokana na tuhuma za kumtukana, hatimaye mbunge huyo ameomba msamaha.

Aprili 4, mwaka huu wakati wa uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mdee alidaiwa kutoa kauli ya matusi dhidi ya Spika Ndugai.

Baadaye kiongozi huyo alitoa amri ya kukamatwa kwa Mdee na kufikishwa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kuhojiwa.

Juzi jioni, baada ya Bunge kupitisha makadirio ya matumizi ya fedha ya Wizara ya Sheria na Katiba kwa mwaka wa fedha 2017/18,  Mdee alimwomba msamaha Ndugai na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalah.

Pia aliwaomba msamaha wabunge, wananchi wa Jimbo la Kawe   na watanzania wote walioguswa na kauli aliyotoa dhidi ya viongozi hao wa Bunge na Serikali na kuhaidi kutorudia .

 “Kwanza nakushukuru Mwenyekiti wa Bunge (Andrew Chenge) kwa kunipa nafasi hii, pia nilitamani wakati nasoma maneno haya Mheshimiwa Spika angekuwapo.

“Lakini ninaamini kuwa uwepo wako unawakilisha kiti cha spika na atasikia neno ambalo nataka kusema hapa,”alisema Mdee.

Alisema Aprili 4, mwaka huu wakati wa uchaguzi wa EALA kuna matukio ambayo yalitokea  yakamsababisha kuzungumza lugha ambayo kwa utamaduni wa Bunge si sawa.

Alisema lugha hiyo husika ilimgusa Spika wa Bunge na Waziri Kigwangala na kwamba akiwa mbunge mzoefu alitumia jitihada kuzungumza na kuwaomba radhi wahusika nje ya viwanja vya Bunge.

Alisema pamoja na kuwaomba msamaha nje ya Bunge lakini akaona busara kwa sababu maneno hayo aliyatoa bungeni hivyo ni vema aombe msamaha huo bungeni.

 “Kwa hiyo niliomba muda huu kwa madhumuni ya kuomba radhi na kumwambia Spika Ndugai namuheshimu na sitarudia.

“Spika ni kiongozi wangu pia ni mwananchi wa Jimbo la Kawe nina kila sababu ya kuzingatia haya mawili kwa umakini mkubwa, hivyo ninaomba radhi kwake, Kigwangala na kwa Bunge,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles