24.1 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

PROF. NDALICHAKO AWAFUNDA WANAFUNZI

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako

 

 

Na MWANDISHI WETU, Kondoa

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Joyce Ndalichako,  amewataka wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana Kondoa,  kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana tija kwa maisha yao.

Aliyasema hayo jana mjini hapa wakati wa mahafali ya kidato cha sita shuleni hapo.

Alisema mitihani si muujiiza kwa mwanafunzi hivyo hawana budi kusoma kwa bidii   waweze kufikia malengo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Waziri aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha wanatumia uhuru wa vyuoni vizuri watakapochaguliwa kujiunga na vyuo kwa vile  maisha ya elimu ya juu hayana ulinzi kama wa shule.

“Napenda kuwasihi sana wanangu kuwa mnapokaribia kumaliza elimu yenu hii ya sekondari na kwenda kujumuika na jamii nendeni mkaendeleze nidhamu na matendo mema ambayo walimu wenu wamewafundisha hapa shuleni.

“Msiende kujiingiza kwenye majanga ya Ukimwi, dawa za kulevya  na sitegemei muende mkapotoke,” alisema Profesa Ndalichako.

Mkuu wa shule hiyo, Flora Nusu, alisema changamoto  zinazoikabili shule hiyo kuwa ni upungufu wa  walimu wa masomo ya sayansi yakiwamo  Fizikia, Kemia, Biolojia, Hisabati .

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,644FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles