25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Haki za wafungwa, mahabusu wawapo gerezani

wafungwa-wanaosubiri-kunyongwa
Wafungwa wanaosubiri kunyongwa.

 

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

HABARI wasomaji wa Haki hainunuliwi, katika ukurasa wetu leo tutaangalia majukumu ya Jeshi la Magereza kwa mahabusu na wafungwa.

Jeshi la Magereza wanasema majukumu ya msingi ya jeshi  ni kuwapokea na kuwahifadhi gerezani watu wote wanaopelekwa gerezani kwa mujibu wa sheria za nchi na kuendesha program zenye kulenga kuwarekebisha wafungwa waliohukumiwa ili watoke wakiwa raia wema.

Kwa mujibu wa waraka ulitolewa na jeshi hilo ni kwamba huduma wanazotoa ni kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Huduma zinazotolewa na jeshi hilo ni kwa ajili ya wafungwa wa aina zote wanaoingia magerezani, ndugu/jamaa za wafungwa, mawakili/wanasheria wa wafungwa, watu wanaotoa huduma mbalimbali kwa wafungwa zikiwamo taasisi zisizo za kiserikali na madhehebu ya dini.

Mfungwa ama mahabusu anapopokelewa gerezani kwa mara ya kwanza anayo haki ya kusomewa taratibu na sheria za magereza zitakazomuongoza awapo gerezani.

Anayo haki ya kuyaeleza matatizo yake kwa uongozi wa gereza, haki ya kupatiwa chakula kulingana na matakwa ya madhehebu yake, haki ya kutembelewa na wakili wake wakati wowote na muda wowote.

Pia haki ya kutembelewa na ndugu ama jamaa zake wakati wowote awapo mgonjwa, ana haki ya kutembelewa na polisi, lakini mfungwa akubali kuonana naye na kwa madhumuni maalumu.
Mfungwa ama mahabusu ambaye ni raia wa  nchi nyingine anapopokelewa gerezani anayo haki ya kupelekewa taarifa za kuwapo kwake gerezani kwa mwakilishi/balozi wa nchi yake aliyepo nchini.

Wafungwa wanayo haki ya kutembelewa na watu wasiozidi wawili mara moja kwa mwezi kwa muda wa dakika 15 au zaidi kwa kibali cha Mkuu wa Gereza na kwa nyakati tofauti.

Inaruhusiwa anapoingia gerezani kwa mara ya kwanza, kabla ya kuhamishiwa gereza jingine, wakati ni mgonjwa mahututi, wakati wowote kwa kibali cha Mkuu wa Gereza kama vile atakavyoona inafaa.

Wafungwa ama mahabusu wanayohaki
ya kutembelewa na wakuu wa dini kwa ajili ya ibada kulingana na madhehebu yake na haki ya kuandika au kupokea barua mara mbili kwa mwezi.

Barua zote zinazotoka na kuingia gerezani ni lazima zisanifiwe au kupitishwa na Mkuu wa Gereza.

Wafungwa ama mahabusu wanayo haki ya kutia sahihi nyaraka kwa mfano hundi, wosia na nyinginezo, haki ya kujiendeleza na masomo ya juu kulingana na sifa zake za awali kitaaluma.
Wanayo haki ya kupata huduma ya malazi na chakula kwa viwango vilivyowekwa na Serikali na haki ya kupata huduma ya tiba na afya kwa ujumla.

Ni wangapi wanajua haki hizo? Ukweli uko wazi kwamba kuna baadhi ya watu hawajui haki za mahabusu na mfungwa anapokuwa gerezani.

Kuna haja ya wadau kuendelea kutoa elimu hiyo ili kila mmoja anayeweza kuingia gerezani, ndugu ama jamaa ajue haki za muhusika ni zipi anapokuwa humo.

Kutojua haki kunafanya baadhi yao kuona kwamba wananyimwa haki za msingi wanapoingia gerezani na kulishushia lawama jeshi hilo.

Ni rai yangu kwa wananchi wasichoke kusoma kwani kushindwa kufanya hivyo kunachangia kutojua haki zenu za msingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles