27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Operesheni ‘tokomeza mzaha wa bodaboda’ inahitajika

img_1409

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

WASOMAJI wa Vituko vya Bodaboda naamini wote mko salama, wale waliokumbwa na madhira nawapa pole nawaombea kwa Mungu awafanyie wepesi katika hayo yaliyowakuta.

Mara kadhaa tumekuwa tukihabarishana kuhusu vituko mbalimbali vya vijana wanaoendesha bodaboda huku tukiwahamasisha kupunguza vituko ili kulinda uhai wao.

Vijana wamekuwa wakiendesha mwendo kasi huku wakisikiliza miziki kupitia simu zao za mkononi kwa wale ambao hawajafunga redio katika pikipiki zao.

Madereva hawa wamekuwa hodari wa kusaka abiria na hawakatai abiria hata kama awe na mizigo inayozidi uwezo wa pikipiki hiyo wao ili mradi waingize fedha bila kujali uharibifu unaoweza kutokea.

Bila kujali amebeba abiria wa aina gani vijana wamekuwa wakifungulia miziki na kuweka ‘headphone’ katika masikio yao ili aweze kusikiliza mziki huku akiwa kazini.

Siamini kama hakuna anayejua kwamba kuwapo kwa kifaa hichio cha kupitisha sauti katika masikio kunapoteza uwezo wa kusikia.

Sidhani kama kuna mtu anayeweza kubisha kwamba kifaa hicho kinaweza kusababisha ajali inapotokea dereva kapigiwa honi ya kuashiria hatari hakusikia kutokana na mziki.

Zakaria anasema vijana wengi wanasumbuliwa na ujana, hawana sababu za msingi zinazowafanya wajizuie kusikia.

“Wanajua madhara ya kuweka kifaa hicho masikioni, liko wazi kwa sababu hata wanapokuwa kijiweni wanaoweka masikioni kusikiliza mziki wakisemeshwa hawasikii mpaka waguswe mwilini.

“Bila kumgusa hata ukimuuliza mlikuwa mnaongea nini hawezi kujibu, ukimuita akaona unamuita anaitika kwa sauti kubwa kama kiziwi,” anasema.

Anasema wanapata ajali nyingi kwa sababu wakipigiwa honi kwa gharura hawasikii matokeo yake kule wanakotakiwa wasiende wanakwenda na kugongwa ama kugonga.

“Mimi napanda pikipiki kwa kuangalia nidhamu ya dereva, siwezi kupanda pikipiki dereva anaimba mwanzo wa safari mpaka mwisho, ukipata dharura huwezi kuwaambia haraka akasikia hadi umshtue kwa kumvuta koti ndipo anapotoa waya wake katika sikio moja akusikilize,” anasema Salim.

 

Salima anasema wengi wangekuwa kama yeye vijana wangeacha kufanya mzaha katika roho za watu, lakini wachache kama yeye ndio waliobahatika kuonyesha hisia zao waziwazi.

Anasema wengi wanakwazika lakini wako kimya, wanajali wfaike safari lakini hawajui iko siku hatafika hiyo safari.

 

Wanapopata ajali ukiuliza majibu ni mepesi kwamba kijana wa bodaboda alikuwa mwendo kasi lakini anasahau kwamba hata abiria hakuwa makini kuhakikisha usalama unakuwapo katika safari hiyo.

 

Watanzania pamoja na haraka tulizonazo tunapaswa kuwa makini na vyombo hivi kwani vinaongoza kwa kuwaacha watu wakiwa walemavu, vinaongoza kwa kuondoa uhai wa watu pia vinaongoza kwa kugonga watu na magari kutokana na kukosekana kwa umakini na haraka walizonazo vijana wanaoendesha bodaboda.

 

Watumiaji wote wanatakiwa kuanza operesheni tokomeza mzaha wa bodaboda kwa kuwa bila ya kufanya hivyo hawataacha na kutokana na kukua kwa teknolojia, vitakuja vitu vingine vitakavyotoa akili na kusababisha vifo vingi zaidi inavyotokana na ajali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles