25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

HAITHAMKIM: USIYEMPENDA KAJA… MTAMKOMA WENYEWE

haitham

Na BEATRICE KAIZA

HAITHAMKIM ni msanii wa kike anayepanda kwa kasi kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, jina lake kamili ni  Haitham Ghazal ambaye yuko chini ya lebo ya MJ Records,

Mrembo huyo ngoma yake ya kwanza inaitwa ‘Fulani’ aliyomshirikisha rapa mkongwe wa Bongo fleva, Mwana FA ambaye inafanya vema ndani na nje ya nchini.

Na sasa anakuja na kazi yake mpya aliyomshirikisha mrembo wa duania Wema Sepetu na kummwagia sifa  lukuki  kuhusu mrembo kufanya  kazi yao mpya ambayo Wema Sepetu ameimba.

‘’Wema Sepetu ni msanii tena anakipaji cha kuimba kama mimi kusema ukweli tumefanya kazi zuri na itakuwa tishio kwa wasanii wa kike ambao wametutangulia kwenye gemu,’’ alisema  Haithamkim.

Ngoma hiyo itwayo ‘PlayBoy’ ambayo ipo jikoni, mwanadada Haitham amesema kuwa tangu aingie kwenye tasnia hii ya muziki hajawai kuona wimbo ambao unampa furaha kila kukicha.

‘’Naomba mashabiki zangu wakae mkao wa kula kwani PlayBoy ni wimbo ambao mwaka 2017 ni lazima upate tuzo, sio kama najisifia hapana ni kutokana na maandalizi ya wimbo huo,’’.

Akizungumza na Swaggaz, mkali huyo anasema kuwa kitu cha kumshukuru Mungu ni lebo yake na prodyuza wake kwa kazi mzuri kwa kumtengenezea wimbo ambao utakuwa ni tishio ya wasanii wa hapa nyumbani.

‘’Daxo Chali ni kiongozi wangu ambaye ananetengenezea ngoma zangu pia kitu cha kujivunia ni kuwa msanii wa kike ninaefanya vema kutokana na MJ Records kunipika vema na kunipa mafunzo ya kutosha katika tasnia hii ya muziki.

Asante uongozi wangu kwa kuniweka katika uangalizi mzuri zaidi ili niweze kufanya kazi nzuri na kutimiza malengo yangu ya kuwa msanii bora ndani na nje ya nchi.

SWAGGAZ: Kwa nini umshirikishe Wema Sepetu na siyo mtu mwingine?

HAITHAMKIM: Kwanza kabisa, aina ya Bongo Fleva ninayoimba mimi ni mpya, unaitwa Tropical House. Baada ya mimi kumaliza kuingiza vocal kwenye ngoma hiyo, kulingana na aina ya wimbo wenyewe, menejimenti yangu ilipendekeza Wema Sepetu akae kwenye ngoma hiyo ndipo itanoga zaidi.

SWAGGAZ: Wema Sepetu anakipaji cha kuimba kweli?

HAITHAMKIM: Nasema hivi kipaji chake  mtakijua kwenye prayBoy siwezi kusema mengi na mashabiki wangu watajionea wenyewe.

SWAGGAZ: Siku ambayo umeambiwa kuwa unakwenda kufanya kazi na Wema Sepetu ulijisikia je?

HAITHAMKIM: Siku ambayo niliambiwa kuwa ninafanya wimbo wangu mpya na Wema Sepetu sikutegemea kuwa atafanya vizuri kama alivofanya, kusema kukweli ni wimbo mzuri zaidi ya nyimbo zote kwani Wema anafanya poa na mimi mwenyewe nimefanya poa zaidi.

SWAGGAZ: Nini kinafanya kichupa cha PrayBoy kisitoke wakati kipo tayari?

HAITHAMKIM: Kichupa kipo tayari, kwa hiyo kinachosubiliwa ni siku ifike, maandalizi yamesha fanyika na video tunatarajia kuiachia mwanzoni kwa mwaka 2017,lakini mitandaoni hasa YouTube itaanza kuonekana hivi karibuni.

 

SWAGGAZ: Sawa ni changamoto gani  ambazo unakutana nazo mara kwa mara katika tasnia hii?

HAITHAMKIM: Changamoto ambayo hadi sasa inanisumbua kichwa ni wakati mwingine ninapokuwa ninasukuma kazi zangu kwenye media kuna baadhi ya watangazaji na Madj ni wasumbufu,  kwani wananitaka kimapenzi pia kwa sababu ninajielewa na ninajua nini nafanya ninaweza kupapana nao na hazinikatishi tamaa.

SWAGGAZ: Kuna tetesi zinasema kuwa unamahusiano ya kimapenzi na Mirror msanii wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Endless Fame inayomilikiwa na Wema Sepetu na h ii ndio imekufanya hadi ukaweza kumpata Wema Sepetu na kuweza kufanya nae kazi?

HAITHAMKIM: Sio kweli mimi na Mirror ni marafiki tu na hatuna uhusiano zaidi ya urafiki na kuhusu Wema ni menejimenti yangu ndio ilimtafuta Wema na sio mimi.

SWAGGAZ: Asante sana Haithamkim kwa ushirikiano wako.

HAITHAMKIM: Asante polisi wa Swaggaz, nakutakia siku njema na kazi njema.

Asante uongozi wangu kwa kuniweka katika uangalizi mzuri zaidi ili niweze kufanya kazi nzuri na kutimiza malengo yangu ya kuwa msanii bora ndani na nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,089FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles