VICTORIA KIMANI ATAMBIA UBORA WAKE

0
522

victoria-kimani

NAIROBI, KENYA

MKALI wa muziki nchini Kenya Victoria Kimani, amedai kuwa kwa upande wake haoni sababu ya kuwashirikisha wasanii wa mbali katika kazi zake, kikubwa ni kufanya kazi bora.

Desemba 4, mwaka huu, msanii huyo ameachia albamu yake ya kufungia mwaka ijulikanayo kwa jina la ‘Safari’, huku akidai kuwa hajawashirikisha wasanii wengi kutoka mbali kwa kuwa anaamini ubora wa albamu unatokana na ubora wa kazi.

“Nimeachia albamu yangu ya Safari, sijawashirikisha wasanii wengi kutoka mbali kwa kuwa ninaamini mwenyewe naweza kuifanya albamu kuwa bora. Siku zote ubora wa albamu unatokana na ubora wa nyimbo zilizopo na siyo kushirikisha wasanii wenye majina makubwa.

“Ubora wangu utanifanya nimalize mwaka huu vizuri na nianze mwaka mpya pia vizuri kutokana na albamu hiyo. Baadhi ya wasanii ambao wapo humo ni Michael Addo ‘Sarkodie’ kutoka nchini Ghana,” alisema Victoria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here