27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

AKOTHEE: MWAKA 2017 NI WA KUOLEWA, KUONGEZA MTOTO

akothee-white-e1476349452130

NAIROBI, KENYA

NYOTA wa muziki nchini Kenya, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Benefactor’ amesema  mapema mwakani atafunga ndoa na kuongeza mtoto.

Msanii huyo mwenye watoto watano sasa, aliwahi kusema kuwa hana mpango wa kuolewa kwa kuwa hakuna mwanamume ambaye atakubali kumuoa akiwa na watoto wengi kiasi hicho, hivyo atapambana na maisha kwa ajili ya kulea watoto wake, lakini anaonekana kufuta kauli hiyo na kudai kuwa mwakani atafunga ndoa na kuongeza mtoto.

“Nimechoka na watu ambao wanapenda kufuatilia maisha yangu, kila mtu ana mambo yake na maamuzi yake, ninachokipanga naweza kukipangua mwenyewe, hivyo sitarajii kuona maneno mengi ya watu.

“Nimepanga mapema mwakani nifunge ndoa, kila kitu kinakwenda vizuri na ninaamini kitakuwa sawa, nina familia ya watoto watano lakini nikiolewa lazima nitaongeza mtoto mwingine,” alisema Akothee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles