28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

FABOLOUS: NAKUJA NA KISHINDO 2017

fabolous

NEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, John Jackson ‘Fabolous’ amewatisha wasanii wa muziki huo nchini humo kwamba mwaka 2017 wanatakiwa wajipange kwa kuwa anakuja kwa kishindo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu, amedai kuwa mwaka 2017 anatarajia kufanya makubwa katika muziki huo kutokana na kukaa kimya kwa muda mrefu.

“Nilikuwa kimya kwenye muziki lakini sikuwa kimya kwenye harakati za maisha yangu, nilikuwa nafanya vizuri kwenye kutafuta fedha, lakini sasa nataka kurudi kwenye muziki kwa ajili ya ushindani.

“Nimekuwa nikiwasilikiza kila siku wasanii wachanga ambao wanafanya vizuri kwa sasa kwenye Hip Hop, hivyo wajiandae nakuja, tangu nimekuwa kimya sijaona msanii ambaye amevaa viatu vyangu katika nafasi yangu, basi nakuja mwenyewe,” alisema Fabolous.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles