Guardiola: Arteta afanye uamuzi sahihi

0
1236

MANCHESTER, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ameshindwa kuzima uvumi wa msaidizi wake kuwa atajiunga na Arsenal hivi karibuni, lakini amemtaka Mhispania mwenzake kufanya uamuzi sahihi.


Guardiola alimjumuisha Arteta katika benchi lake la ufundi pindi alipojiunga kwa mara ya kwanza na kikosi cha Manchester City msimu wa 2016/17, wakati huo alikuwa ametoka kustaafu soka akiwa na Arsenal.


“Siwezi kusema anaondoka au anabaki, lakini naweza kumuelezea kama mmoja wa watu wazuri wanaojua majukumu yao, kimbinu na mambo mengine yote.


“Kwa sasa yupo hapa, ingawa, najua kulikuwa na maongezi kati yake na Arsenal, atulize kichwa afanye uamuzi sahihi,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here