27.1 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mendes: Ronaldo hawezi kuondoka Juventus

TURIN, Italia

WAKALA wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes ameweka wazi msimamo wa mteja wake kuwa hana mpango wa kuondoka ndani ya kikosi cha Juventus baada ya msimu huu kumalizika.


Ronaldo alijiunga na mabingwa hao wa Italia msimu uliopita akitokea Real Madrid kwa dau la pauni milioni 88 (bil. 269 za Tanzania) na kuwa mchezaji ghali zaidi ndani ya wakali hao wa Ligi Kuu ya Italia, Seria A.


Hivi karibuni kulikuwa na tetesi nyingi zilizomuhusisha supastaa huyo wa Ureno kutaka kuondoka sababu ya kukosa furaha chini ya kocha mpya wa Juventus, Maurizio Sarri aliyekuwa akikinoa kikosi cha Chelsea msimu uliopita.


Pia, Ronaldo ambaye aliitumikia Real Madrid kwa miaka tisa, mkataba wake na Juventus utafika tamati mwaka 2022, imebainika maongezi ya mkataba mpya yataanza hivi karibuni chini ya wakala Mendes.


“Cristiano anafuraha kuwa hapa, hawezi kwenda kokote hana rekodi hiyo ya kuondoka mapema katika timu anazocheza, miaka sita alikaa Manchester United, tisa aliitumia Real Madrid hata Juventus anataka kuwa kwa muda mrefu.


“Kusema kweli hatufikirii kusikiliza ofa nyingine zaidi ya kuongeza mkataba hapa, anavutiwa zaidi na mipango yao anahitaji kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Juventus,” alisema.


Itakumbukwa Ronaldo anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani sambamba na Lionel Messi wa Barcelona, Mreno huyo amefanikiwa kushinda tuzo tano za Ballon d’Or.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles