Papa aondoa kanuni iliyokuwa inafunika siri za kashfa za kingono

0
741
Papa Francis

ROME, ITALIA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameondoa kanuni iliyokuwa inafunika siri juu ya kashfa za udhalilishaii wa kingono ndani ya kanisa hilo.

Papa Francis amechukua hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kwamba kanuni hiyo ilikuwa inatumika kwa ajili ya kuwalinda wahalifu na kuwanyamazisha waliofanyiwa uhalifu wa kingono na pia ilitumika kuwazuia polisi kuchunguza uhalifu huo.

Watu waliotendewa uhalifu huo wa kingono pamoja na mawakili wao wameushangilia uamuzi wa Papa Francis na kwa mtazamo wao, hatua hiyo ilipaswa kuchukuliwa mapema zaidi.

Hata hivyo wametahadharisha kwa kusema kwamba ufanisi wa hatua hiyo utathibitishwa pale ambapo kanisa litakapolazimishwa kukubali uchunguzi ufanyike katika nchi husika na nyaraka zote juu ya wahalifu zitolewe hadharani.

Kwa mujibu wa sheria mpya Papa Francis ameeleza kuwa habari zinazohusu uhalifu wa kingono zitalindwa na viongozi wa kanisa lakini ameeleza wazi kwamba kanuni ya kanisa kuficha siri haitatumika tena

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here