29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Guardiola amtaka Toure aombe msamaha

pep-guardiola-yaya-toureONDON, ENGLAND

KOCHA  wa  timu ya Manchester City,  Pep Guardiola, amesema hatompanga  katika kikosi chake kiungo wake, Yaya Toure, hadi  wakala wake  atakapoomba msahama kutokana na kukosoa uamuzi wake  wa kumweka  nyota huyo benchi.

Tangu msimu wa Ligi Kuu England uanze, kiungo huyo amecheza mchezo mmoja pia alitemwa katika kikosi kitakachocheza michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Wakala wake, Dimitri Seluk, alidai kuwa  kiungo huyo alidhalilishwa na kocha wa timu hiyo.

“Seluk  lazima aombe msamaha, kama hatofanya hivyo Toure hatocheza katika kikosi change,” alisema.

Lakini Seluk aliiambia BBC Sport kuwa hana kitu cha kuomba msamaha kama ambavyo kocha  huyo  anavyodai.

“Anatakiwa kuzungumza na Yaya ambaye anafanya kazi yake, hata hivyo tutaona nini kitatokea kwa kuwa nyota huyo anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu ambapo Januari mwakani atakuwa huru kuondoka,” alisema Seluk.

Guardiola ambaye aliwahi kuifundisha timu ya Barcelona wakati Toure  akiuzwa timu ya Manchester City mwaka 2010.

“Ilikuwa ngumu kumwacha  katika kikosi changu kitakachocheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, namjua vizuri lakini baada ya wakala wake Seluk kuzungumza, nikamtoa nyota huyo kwenye kikosi changu.

“Kitendo alichofanya wakala wake sikubaliani nacho, nikiwa kama kocha wa timu hii, wakati mchezaji hachezi hakuna haja ya kwenda kwenye vyombo vya habari na kuzungumza ovyo ovyo,” alisema Guardiola.

Guardiola alimtaka wakala wa nyota huyo kutumia  pia vyombo vya habari kuomba msamaha kwa kitendo alichofanya ndipo ampange  kiungo huyo katika kikosi chake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles