24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

GGML wadhamini mkutano mkuu wawanajiolojia Arusha

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kuunga mkono ukuaji wa fani mbalimbalinchini, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imejitosa kudhamini mkutano mkuu wamwaka wa wanajiolojiawa Tanzania unaofanyika mkoani Arusha.

Mkutano huo ambao umeanza tarehe 4 Oktobaunatarajiwa kumalizika Oktoba 7, mwakahuu na unaratibiwa na Chama cha Watalaamwa Jiolojia Tanzania (TGS) kinachokadiriwa kuwa na wanachama zaidi ya 300.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Mrakibu waJiolojia katika Kampuni ya GGML, Eric Kalondwa alisema ampuni ya GGML imetoashilingi milioni 25 za Kitanzania kudhamini mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko kwa niaba ya Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango lakini unatarajiwakufungwa na Waziri wa Maji, Juma Aweso.

Alisema katika mkutano huo ambao hufanyikakila mwaka kwenye mikoa tofauti tofauti, jumlaya wanajiolojia 11 kutoka mkoani Geita wameshiriki. 

Aliongeza kuwa mkutano huo umelengakubadilishana uzoefu kwa sababu kunaprogamu mbalimbali zinazolenga kuwawekapamoja watu wenye fani zinazofanana.

Alisema wafanyakazi wa GGML ambao pia niwana fani hiyo ya jiolojia, wamefaidika kwanamna mbalimbali tangu kianzishwe chama hicho.

Alisema mkutano wa mwaka huu unalenga kukazia suala la upatikanaji wa bodi ya wanajiolojia hasa ikizingatiwa fani hiyo inajumuisha watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwamo wanaofanya kazi kwenye uchimbaji wamafuta, kwenye maji, madini ya aina mbalimbalitofauti na dhahabu.

Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa changamoto yauhaba wa wanawake kusomea fani hiyo, lakiniakawatia shime wanawake kusomea fani ya jiolojia kwani haihitaji kuwa  na nguvu kubwa ili kukidhi vigezo vya kuwa mwanajiolojia.

“GGML kwa kweli inafanya vizuri sana kuendeleza ma jiolojia toka wanapokuja kujifunza kwa  vitendo na wanaokuja kazini.

“Wale wanaopitia kwenye mgodi wetu hakika wanawasifia kwa mapokeo makubwatunayowapatia kulingana na program ya mwaka ambayo huwa tunawaandalia,” alisema.

Wanajiosayansi ni wataalam waliosomea nawenye uzoefu wa fani za jiolojia (miamba), jiofizikia, jiokemia, jioteknolojia na jiolojia yamazingira na nyinginezo.

Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa madiniDk. Biteko alisema wizara iko katika hatua za mwisho  za kukamilisha mchakato wakuanzishwa kwa  bodi ya wanajiolojia  na kuongeza kwamba, baada ya Serikalikukamilisha  sehemu yake, itatoa nafasi kwa  wadau kutoa maoni kuhusu namna gani bodihiyo iundwe, namna itakavyo simamiwa,  masuala yatakayohusisha vyanzo vya fedha nakuangalia masuala ya sheria.

Aliongeza kuwa, wakati Serikali inakamalimishamchakato wa kuundwa kwa  bodi yawanajiolojia ni muhimu wajiolojiawakahakikisha wanaiendeleza taaluma ya jiolojia ili kuipatia nchi heshima ikiwemo kuwawezesha wawezekaji kupata taarifa sahihi na hivyo kuvutia uwekezaji zaidi kwenye sektaya Madini.

Pia aliwataka Wajiolojia nchini kuhakikishawanaiheshimisha taaluma yao kwa kutoruhusuwasio waaminifu kuingilia majukumu yakitaaluma kutokana na umuhimu wa shughuliza utafiti kwa maendeleo ya Sekta ya Madini naTaifa.

Aidha, Rais wa Chama cha Wataalam wajilojiaTanzania, Prof. Abdulkarim Mruma aliieleza hadhira kuhusu utajiri wa kijiolojia ambao nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa nao na kuelelezea namna bora ya kuitumia taaluma hiyo kwa maendeleo ya nchi na jamii nzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles