26.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Halotel yasherehekea miaka 7 ya utoaji huduma kwa kuchangia damu

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu ya Halotel na wafanyakazi wake leo wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea na kuadhimisha miaka saba ya utoaji wa huduma za mawasiliano.

Halotel imefanya zoezi hilo ikiwa ni moja ya taratibu ambazo kampuni imejiwekea kama msaada wa kumrudisha shukurani kwa jamii pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali kupitia sekta ya afya katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu katika hospital na vituo vua huduma za afya.

Sehemu ya Wafanyakazi wa Halotel.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Dar es Salaam leo Oktoba 7, 2022, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Sakina Makabu, amesema kuwa ili kuhakikisha tunasaidia Sekta hii ya Afya nchini, ni vyema kuchangia damu na kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji damu.

“Kwa kupitia takwimu za Wizara ya Afya inaonyesha kuwa kuna uhitaji wa damu kwa mama wajawazito, wototo, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji, hivyo kwa kushirikiana na taasisi ya tiba ya Mifupa Mhimbili (MOI) tumeendeleza huduma hii kama hitaji maalum na ishara ya upendo kwa vitendo kwa watanzania amabao ni wateja wetu.

“Tunatambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekata ya Afya hasa katika upatikanaji wa damu, kwa wagonjwa na kuamua kwa kuendelea kuunga juhudi za utatuzi wa changamoto hii kwa kujali umhimu kama Kampuni na wafanyakazi tumeamua kurudisha upendo kwa jamii,” amesema Sakina.

Aidha, mmoja wa wafanyakazi waliochangia damu, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mtandao, Dalili Musa, amesema kuwa, ni furaha kwa kuwa zoezi hilo linaweza kuonekana dogo lakini linaweza kuokoa maisha ya wateja wao na Watanzania kwa ujumla 

“Tunajukumu la kurudisha upendo kwa watanzania na wateja wetu kitu ambacho kitaleta tabasamu kwa wahitaji wote wa damu na kuokoa maisha yao,” amesema Musa.

Kwa Upande wa uongozi wa MOI, Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo, Patrick Mvungi, amesema kuwa wamefarijika kwa zoezi hilo na kampuni ya Halotel pamoja na wafanyakazi wake kwa kushiriki katika zoezi kubwa la utoaji damu huku akiomba liwe endelevu ili kuleta ushirikiano katika sekata ya afya .

“Tunatoa rai kwa taasisi mbalimbali kuweza kujitoa na kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwa kuleta ushirikiano katika sekta ya afya ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu katika benki ya taifa ya damuna hospitali mbalimbali nchini ili kuweza kuokoa maisha ya watanzania,” amesema Mvungi.

Aidha, licha ya kampuni ya Halotel kupiga hatua katika kusambaza huduma za mawasiliano na Intaneti yenye kasi ya 4G maeneo mengi nchini, pia imekuwa ikijihusisha kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya Watanzania, hii ni katika kuonyesha kuwa inathamini jamii ya watanzania kwa nyanja mbalimbali ikiwemo kuboresha sekta ya afya na nyinginezo kama moja ya kipaumbele cha Kampuni kwa maendeleo ya watanzania na nchini kwa ujumla

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,560FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles