24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

FURSA, CHANGAMOTO ZA HAKIMILIKI KWA WATUNZI WA VITABU

Wadau wa walioshiriki semina ya kujadili hakimiliki, wapili kulia ni Mkurugenzi wa Biashara za Nje, Wilson Malosha na wa kwanza kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa KOPITAN, Angel Edmin.

 

 

Na Abdullah Saiwaad na Praxeda Kimath

KILA Aprili 23, wadau wa Vitabu na Hakimiliki huadhimisha Siku ya Vitabu na Hakimiliki Duniani (World Book and Copyright Day). Hujadili kuhusu vitabu, hakimiliki na kufanya maonesho ya vitabu. Aprili 26 ya kila mwaka wadau wa miliki bunifu husherehekea siku ya Miliki Bunifu Duniani (World Intellectual Property Day).

Kwa kuwa shughuli hizi zimefanana na wadau ni walewale, na kwa kuwa  Aprili 26 ni siku ya Muungano, Chama cha Haki nakili (KOPITAN) kikiwashirikisha Chama cha Haki miliki Tanzania (COSOTA) wameadhimisha na kusherekea sikukuu hizi mbili kwa pamoja Aprili 27 mwaka huu. 

Sherehe hizo kwa kiwango kukuona zilifadhiliwa na IFRRO (International Fedaration of Riproduction Rights Organization). KOPITAN ni mwanachama wa muunganiko wa vyama vya Haki nakili duniani. Maktaba Kuu ya Taifa ni sehemu iliyofanyika sherehe hiyo. Ilikuwa sehemu muafaka kwa kuwa maadhimisho yalifanyika katika eneo ambapo hakimiliki inathaminiwa.

Mgeni Rasmi alikuwa ni Wilson Malosha ambaye ni Mkurugenzi wa Biashara za Nje, aliyemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara inayosimamia sheria ya Hakimiliki. 

Akifungua semina hiyo, Malosha alieleza kwa kirefu umuhimu wa kusoma vitabu duniani. Alieleza mchango wa vitabu katika maendeleo ya nchi na akaeleza umuhimu wa kutunza vitabu hivyo dhidi ya uharamia.

Alisema wazi kuwa kurudufu kazi za waandishi wa vitabu bila idhini ya waandishi na wachapishaji wa vitabu ni wizi sawa na uharamia. Alisema kutunza hakimiliki itasaidia kupata waandishi bora wengi zaidi watakaoandika vitabu  bora ambavyo vitatumika kwa ajili ya kujifunzia ili kujenga taifa lililoelimika.

Pia aliwapongeza KOPITAN kwa jitihada kubwa wanazotumia kuhakikisha wanasimamia vyema kazi za waandishi. Kazi za KOPITAN ni kuhakikisha kuwa kazi za watunzi zinazolindwa na hakimiliki hazirudufiwi bila idhini kutoka kwa watunzi. Pamoja na changamoto nyingi wanazokutana nazo wizara iliahidi kupitia COSOTA watatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kazi za wasanii wa maandishi zinalindwa katika misingi inayotakiwa.

Mtoa mada Moses Range ambaye pia ni Ofisa Leseni kutoka COSOTA aliichambua Sheria ya Haki Miliki Tanzania (1999). Alianza kwa ufafanuzi juu ya hakimiliki na haki shilikishi, akisema hakimiliki ni ulizi wa kisheria kwa mtunzi wa kazi halisi. Ulinzi ambao hujitokeza katika makundi mawili, moja haki za kiuchumi na pili haki za kimaadili.

Alisema hakishiriki ni haki zinazohusu matumizi ya pili ya hakimiliki ambazo wasanii wanastahiki.

Alieleza vitu ambavyo hulindwa na sheria ya hakimiliki na kwa muda gani. Alifafanua kuwa kitu kikishapewa ulinzi wa hakimiliki, basi hairuhusiwi kuigwa au kukitoa kwa jinsi yoyote bila ya idhini ya mtunzi.

Vilevile alieleza adhabu za kuvunja sheria ya hakimiliki. Alieleza pia haki inavyoweza kugawiwa kwa ajili ya kuimiliki kiuchumi. Lakini pia alieleza kuwa haki ya kimaadili haiwezi kutolewa kwa mtu mwingine. Akiimaanisha kuwa kazi ya hakimiliki ya mwandishi fulani itabaki yake hata kama ameuza haki zote za kiuchumi za kazi hiyo.

Adhabu hiyo inaweza kugusa taasisi inayokiuka hakimiliki na vilevile anaweza kushtakiwa mfanyakazi katika taasisi. Range akaelezea kazi za COSOTA kuwa ni kusajiri kazi za wasanii, kulinda na kutatua migogoro ya wasanii lakini pia changamoto wanazokutana nazo ni kuwapo na uelewa kidogo kwa wasanii na hakimiliki na pia elimu duni kwa jamii juu ya haki za wasanii na kazi zao.

Mada ya pili ilitolewa na Ofisa Leseni kutoka KOPITAN, Praxedah Kimath ambaye alichambua maana ya kurudufu kazi. Kisha akaeleza athari za kurudufu kazi za waandishi bila kibali kuwa husababisha waandishi kukosa hakimiliki za kazi zao ikiwa ni haki ya kiuchumi na kimaadili na kuvunjwa moyo wa kuendelea na kazi ya uandishi.

Ukosefu wa elimu kwa wadau wote ilionekana sababu ya watu kuvunja sheria na kurudufu kazi za waandishi bila idhini. Alieleza kazi kubwa inayofanywa na KOPITAN na kuhakikisha haki za waandishi zinalindwa na wananufaika na kazi zao.

Aliwasihi waandishi kutokata tamaa kuandika vitabu kwa sababu ya hasara kubwa wanayoipata pale ambapo kazi zao zinarudufiwa au kutolewa kopi.

Aliwatia moyo kuwa kanuni zilizoandaliwa kwa ajili ya kusimamia haki zao zitafuatwa na watanufaika na kazi zao kulingana na kanuni zinavyoelekeza.

Mchapishaji wa vitabu kutoka PATA, Abdullah Saiwaad naye alipata nafasi ya kuongelea Sheria ya Hakimiliki hasa kuhusu ruhusa na mipaka.

Katika Sheria ya Hakimiliki, ruhusa hutolewa kutumia kazi za hakimiliki bila kusubiri idhini ya mwenye hakimiliki. Hiki ni kipengele cha 12 katika Sheria ya Tanzania.

Alifafanua kuwa kipengele cha 9 kinachompa haki mwenye hakimiliki hairuhusu kazi hiyo kufanyiwa lolote. Kipengele cha 12 kinatoa mwanya kwa masharti.

Masharti hayo yanayoitwa mtihani wa hatua tatu. Mtihani huo ni kwa kadri ilivyokubaliwa na watia saini wote wa Mkataba wa Berne wa ulinzi wa haki miliki, Mkataba wa Shirika la Kimataifa la Mali Bunifu (WIPO) na wa Jumuiya ya Kimataifa ya Biashara (WTO).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles